Ajira za siri za Mahakimu kutoka Tume ya Utumishi wa Mahakama

Jun 17, 2024
12
14
Tangu kuanzishwa kwake, Tume ya Utumishi wa Mahakama imekuwa ikitangaza rasmi ajira za Mahakimu na kuwachagua wale waliofuzu na kukidhi vigezo stahiki kwa tangazo maalumu na kwa uwazi.

Lakini hivi majuzi mnamo tarehe 20 Septemba 2024, Jaji mkuu ameapisha mahakimu 22 ambao baadhi yao hawakutangazwa popote kwamba wamechaguliwa kwa namna gani au kwa vigezo vipi.

Tunatoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika kuangalia huu utaratibu uliotumika ni utaratibu wa aina gani?

Kama uko sahihi ni sawa? Lakini kwanini siri?

Hata majaji wanapoteuliwa na Rais wanatangazwa hadharani kila mtu anawajua, kwanini hawa mahakimu wamechaguliwa na kuapishwa kwa uficho?

Mamlaka zinazohusika tafadhali tunaomba tochi zenu ziangaze hiki kichaka.
 
Mihimili yote nchini imeingiliwa na wahuni.

Tuendelee kuombea utawala bora utamalaki Tanzania.
 
Hao mahakimu waliapishwa kimya kimya wakipigiwa zile simu alizosema Rostam wanakuwa watiifu kwa simu kuliko haki za raia
 
Back
Top Bottom