Salamu kwako wewe uliechaguliwa kupitia mfumo wa TCU lakini huna uhakika kama kile ambacho umekisoma unaweza pata ajira serikalini ama katika taasisi ambazo si za kiserikali.
Tangu nilipoanza chuo pale Kampala international university kwa kozi ya conflict resolution and peace bulding mbayo nilipata kuchaguliwa kwa kupitia mfumo ule TCU sijawahi kuona hata siku moja serikali ama taasisi binafsi zinatangaza kuwa zinahitaji kuajili watu waliosomea shahada hii. Nilikuwa nikisaka sana nakukuta ni Umoja wa Mataifa na taasisi nyingi ambazo ni za nchi nyingine haswa baani Ulaya.
Nimeanzisha uzi huu kukukaribisha wewe uliyesoma kozi yoyote ile ambayo hukuwahi kusikia wakiitangaza kuwa wanataka kuwaajiri mtu kama wewe. Nadhani hili kwa namna moja ama nyingine itaweza kukumbusha serikali/taasisi nyingine kuwa kuna watu kama sisi.
Pia itawakumbusha TCU kama waliweza kuruhusu wanafunzi kuchagua kozi walizoziorodhesha ina maana kuwa hata serikali ama taasisi nyingine zitatoa ajira hizo.
Basi sasa weka kozi yako hapo chini kuikumbusha serikali kuwa kuna watu kama sisi ambao waliorodhesha kozi.