Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 904
- 2,516
Kijana William Bahati (20) Mkazi wa Kijiji cha Kashero Wilayani Mbogwe Mkoani Geita amefariki Dunia kwa kujinyonga na kamba ya kufungia mbuzi huku sababu zikitajwa kuwa ni kukosekana kwa nauli ya kwenda ukweni kumzika Baba Mkwe wake.
Akiongea kuhusu tukio hilo Mke wa Marehemu, Grace Jeremiah Mkazi wa Kijijini hapo amesema sababu za Mumewe kujinyonga zimetokana na kushindwa kupata nauli ya kwenda ukweni ambako kulikuwa na Msiba wa Mkwewe .
"Mume amejinyonga baada ya kukosa nauli ya kwenda msibani nyumbani kwetu, tulikuwa ndani mida ya saa 11 akawa anasikitika kuwa anaumia kukosa nauli ya kusafiri yeye na Mimi kwenda kumzika Baba, sasa aliamka kitandani akavaa nguo akatoka akasema ngoja niende shambani ndio tukamkuta sasa ameshajinyonga”
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kashero Alfred Msukuzi amesema tukio hilo limetokea October 2 mwaka huu ambapo amekiri kuwa Kijana huyo amejinyonga kwa kukosa pesa ya kwenda ukweni.
#MillardAyoUPDATES