Ajaribu kutazama tamthilia za kikorea, labda zitampa mafunzo!

Hyungnim

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
301
482
"Huwezi kugawa chakula ardhi ni nyeu...ya kijani hivi.Hakuna chakula cha serikali kwani serikali haina shamba!Sileti chakula.Kuna ambao tetemeko lilibomoa nyumba zao kdg wakadanganywa serikali itawajengea mwafwaa(mmekufa)!

Ukitazama vema tamthiliya za kihistoria za kikorea hasa zile za kifalme utagundua kauli kama hiyo hapo juu ya kifedhuli usingeiona kwa kiongozi mzuri.Hata mchakato wa kumpata mfalme mpya ulizingatia vigezo vingi.Navyo ni busara,uvumilivu,anavyodhibiti jazba,upendo wake kwa watu wa kawaida na utu!

Nitatumia baadhi ya mfululizo wa tamthiliya kama rejea.

Ktk tamthiliya ya JUMONG prince chumong anapendwa na watu wengi akiwemo mfalme Geumwa/Kumwa ingawa hakuwa baba yake mzazi!Mfalme antamani kijana huyo ndio awe kiongozi wa Buyeo kuliko wanawe yaani prince Daesso na Young po!walikuwa watu wenye chuki,dharau,tamaa hivyo hawakufaa!Daesso anachukua madaraka kwa nguvu.Kinachotokea ni kutesa wapinzani wake kwa kuua na kuwasweka jela!Mkono wa chuma.

Chumong anaamua kuanzisha himaya yake kwingineko akiwatumia wafungwa waliokombolewa!Himaya inaimarika.Neema zinabubujika!Chumong hakuwa mjivuni.Aliishi vzr na watu wa kawaida.Mo palmo mtengeneza panga,Musong mlinzi wa pango na rafiki zake wa karibu.Aliheshimu ushauri wao.Wakawa ndugu zake.Hakuwatisha.

Pia ktk tamthiliya ya Hong Gil Dong,mhusika mkuu Gil Dong ingawa hakuwa na uwezo wala uongozi anawajali wanyonge!Yeye pamoja na wanyang'anyi wenzake wanakwiba chakula kwa matajiri ambao utajiri wao umetokana na kunyonya jasho la kapuku kisha wanawagawia maskini chakula hicho.Mfalme hakahangaika na matatizo ya watu.Alizungukwa na starehe za pombe na wanawake!

Pia Kijana Iljimae ktk the return of Iljimae na Iljimae yenyewe anawatia adabu watesi wa wananchi!anakwiba fedha na chakula kwa mabwanyenye na kukisambaza kwa maskini!Kwakuwa viongozi waliamua kila raia aubebe msalaba wake wabaharakati hao wanaamua kubeba jukumu la kuwapa shibe wananchi!

Je huyu wakwetu hawezi kuelimika akiziona hizo?nakwakuwa zinaigizwa kwa hisia nzito pengine anaweza kuguswa!shingo asiishupaze!

Niishie hapa..nimeandika kwa hofu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…