Ajali za Bodaboda ni janga la taifa. Ajali nyingi kwa Dar ni Barabara ya Bagamoyo maeneo ya Mbezi Beach, Tegeta na Goba

Lady Mwali

Senior Member
Nov 15, 2018
147
333
Kwa kweli wadau wa JF ajali za Bodaboda boda zitatumaliza.

Kwa muda mfupi jijini Dar es Salaam kumetokea vifo vingi na ulemavu vilivyosababishwa na ajali za bodaboda.

Usafiri huu unapendwa sana na akina dada lakini ni hatari sana kwani madereva wengi wa bodaboda hawana leseni na hawafati sheria za barabarani.

Mc.Pilipili kapoteza mama yake mzazi na mama yake mdogo katika ajali ya bodaboda katika eneo la Mbezi Beach.

Hukohuko Mbezi Beach kuna ajali nyingi sana za bodaboda mpaka Tegeta, Bunju na maeneo ya Bagamoyo.

Kwa nini huko kuna ajali nyingi sana za bodaboda?

Hivi majuzi tuu ajali ya bodaboda imepoteza maisha ya dalali maarufu sana hapo Mbezi Africana. Dalali huyo anajulikana kwa jina la Mudhihiri. Amekufa kifo cha ajali ya bodaboda akiwa kama abiria, gari iliwagonga kwa nyuma.

Chondechonde imetosha, bodaboda zitatumaliza ifike wakati serikali ipige marufuku usafiri wa bodaboda kunusuru maisha ya Watanzania au kwa kuwa nyinyi viongozi hamguswi na ajali ya bodaboda?

Mbona Zambia wamepiga marufuku bodaboda kubeba abiria kibiashara.

Maisha yetu yana thamani kuliko kitu chochote.

Kwani hata kirefu cha BODA chaweza kuwa;

B= Beginning
O=Of
D=Death and
A=Accident.

Wabunge tunaomba mkapaze sauti bungeni ili sheria iliyoruhusu bodaboda kubeba abiria ibadilishwe kwani sheria hii imepitishwa kisiasa ili kupata kura nyingi za vijana ambao wengi wao ni madereva wa bodaboda. Kama bodaboda usafiri wa maana mbona wabunge wanatembelea na V8 na sio bodaboda?

Nawasilisha.
 
Mmejipanga vipi bodaboda ni jeshi kubwa sana huwenda hata ni karibu milioni mbili

Sasa aina ya hawa madereva kwa asilimia kadhaa bodaboda imewaondoa kwenye life style isiyofaa kwenye jamii

Unapoirudishia jamii watu milion mbili wasio na ajiraWatu wenyewe ni aina ya madereva wa bodaboda ni janga kuliko ajali za bodaboda zenyewe

Boda zimerahisisha maisha sana

Maisha yatakuwa magumu siyo kwa madereva tu lakini hata kwa watu wengi ambao wanazitegemea hizo boda kwenye shughuli zao za kila siku

Zambia ni nchi Tanzania pia ni nchi siyo lazima tuige walichofanya zambia ndiyo tuwe sahihi

Kutafuta njia ya kudhibiti ajali ni rais zaidi ya kusitisha shughuli za bodaboda




Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom