Tatizo ni ugumu wa wafiwa kuweza kujua kama marehemu alikuwa na pesa ama la....na zaidi wengine huwa na line maalumu kwa ajili ya tigo pesa/mpesa ambazo ndugu pengine sio rahis kuzijua. Lakini kwa vyovyote vile kama ilivyo kwa ma benki, nadhani lazima kuna utaratibu wa kuzipata (kwa kuzingatia sheria za mirathi nk).
Lakini najiuliza pia zile walizokuwa nazo mifukoni (ambazo kwa wafanyabiashara aghalabu huwa nyingi pia) wafiwa watazipataje?