Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Watanzania tungekuwa wamoja tuhakikishe wahusika wa shule hii wanawajibishwa kwa vifo hivi Na ukizingatia hata RPC anatoa taarifa za uongo kuwa ni wanafunzi 30 wakati ni zaidi ya 33
 
Hivyo ni aibu kwa taifa Na nijinsi gani kuwa serikali haipo makini wananchi tusoposhikamana tutaishia pabaya sana
 
Mkuu,ukisema ajali haina kinga unakosea sababu kwa uelewa wangu 80% ya ajali husababishwa na binadamu pamoja na mazingira na 20% ni sababu ya chombo husika,hivyo kama mtumiaji wa chombo cha moto akiwa makini kuanzia kwenye ukaguzi wa chombo kabla na baada ya safari,na pia kuondoa udereva wa mazoea sidhani kama kuna kitu ambacho kitashindwa kuepukika,pia hata ikitokea ajali basi impact haitokuwa kubwa kiasi hicho
 
Kuna Point Kiasi Ndani Yake
Sio kiasi mkuu hizo zote points,ukitaka kuamini kama wewe mkazi wa mji wa Dar angalia zile school buses zinazozunguka mjini zinavyojaza watoto.unakuta zimepakia tutoto twingi mpaka twingine tumepakatana madereva wenyewe nusu wendawazimu maana unakuta dereva anakimbizana na madereva wa daladala gari yenyewe model za 90's inatembea upande upande kama imekatika center bearing huku kabeba watoto wadogo wa shule inayotamba kutoa elimu nzuri sasa hapo likitokea la kutokea ndo kama hivi.
 
Serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya nchi itoe waraka wa kuhakiki vyombo vya moto hasa magari ya wanafunzi katika shule binafsi.

Haiwezekani wazazi
/walezi wanalipa mamilioni ya fedha alafu wamiliki wa shule wanaishia kuwa na magari mabovu ya wanafunzi.

Ni jambo LA ajabu kabisa kukuta wanafunzi wamerundikwa kama magunia kwenda shule na kurudi nyumbani.

Sawa tunaweza sema ajali haina kinga,lakini ajali nyingine ni uzembe unaotokana na wamiliki wa shule zetu za binafsi nchini.

Tafadhali wamiliki wa shule huduma zenu ni mzuri,lakini mengi ya magari yenu ni mabovu au ni Yale ya kukodisha kwa watu.

Tengeni fedha kununua magari mengi na mazuri yanayotosheleza mahitaji ya wanafunzi mlionao.
 
acha unafiki walikuwa wangapi kwenye gari
Kwa hiyo hautaki ukaguzi wa magari ya wanafunzi katika za binafsi yakaguliwe kama yana ubora?

Ni lini coster ikabeba watu zaidi ya 25?

Au kwa sababu ni wanafunzi wanaweza bana bana.

Tuwe wakweli hakuna MTU anayependa unafiki,Mara nyingi matatizo yanafunza kitu Fulani na kurekebisha makosa yaliyopo.
 
Una hoja ya msingi, kwa uelewa wangu mimi, ajali zinazotokea kwa sababu ya makosa ya kibinadamu ( ambayo ndio inachangia zaidi ya 70%), ubovu wa chombo ( mechanical failure) na ubovu wa miundombinu, tusubiri report ya uchunguzi ili tujue ukweli
 
Mawazo yako kama ya Mpiga ramli chonganishi hayo uliyoeleza ya uhusiano gani na hii ajali? Maana hata gari ingekuwa Mpya bado ajali inaweza kutokea.

Hapa cha kulaumu ni barabara zetu tu na si kingine
 
Kwa kuwa we continue to point our fingers towards the wrong direction,tutaendelea kuangamia day in and day out.Very sad.Sijui kwa nini we are so afraid to confront our real enemy,the Devil and his agents who are all around us.
 
Ni ukweli usio pingika hawa jamaa wa mashule wanatumia magari mabovu sana, niwakati umefika serikali kuliangalia kwa umakini mkubwa hili swala
 
Ndugu umekosea sana bara bara iko sawa haina tatizo ina alama za barabarani zote inasafirisha 90% ya watalii wote wanaokuja kanda ya kasikazini hawapati ajali sababu madereva wameenda shule Na magari siyo mabovu usitetee ujinga kwa imani potofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…