LGE2024 Aisha Madoga: Mchague viongozi wanaojali maslahi ya wananchi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,103
2,633
Wakati kmpeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zikiwa zinaendelea kurindima nchini na vyama vilivyosimamisha wagombea vikiendelea kuomba ridhaa kwa wananchi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Dodoma kupitia kwa Mwenyekiti wake, Aisha Madoga kimeendelea kunadi wagombea katika mitaa na vijiji mbalimbali ambapo akiwa wilayani Bahi amewataka wananchi kuchagua Viongozi wanaojua haki na maslahi ya wananchi, wenye uwazi katika miradi, wanaoitisha mikutano ya kijiji kwani wameshuhudia katika kipindi cha miaka mitano kumekuwa na viongozi wa vijiji wasiowajibika.

Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Aidha amesema kwa kuwa CHADEMA inaamini katika haki, ni vyema wananchi kutimiza wajibu wao wa kupiga kura ili kupata haki kwani maisha yao yapo kwenye serikali ya mitaa.

 
Back
Top Bottom