N:B: Ni muhimu kupima Network kwenye eneo lako kabla ya kununua kuzuia hasara.
Haya mambo ya kununua vifurushi vya buku buku unaweza kujikuta unaunga mara 3 na zaidi kwa siku, haba na haba hujaza kibaba mwisho wa mwezi umechoma 80k hadi laki kwenye bando
Suluhisho ni huduma ya unlimited internet, Hulipii Gb unalipia speed,
Kuna unlimited ya waya inaitwa fibre, kuna kampuni kama Zuku fibre, Halotel fibre, Ttcl fibre, Tigo / Yas fibre, n.k. unavutiwa waya mpaka nyumbani lakini changamoto yake huwezi kutembea nayo, ipo maeneo machache ya mjini na umeme ukikatika kifaa kinazima.
Makampuni ya simu wakaleta unlimited internet unayoweza kuhama nayo lakini changamoto ilikuwa gharama , Mfano Vodacom na Tigo kifaa (router) cha bei ya chini ni 250,000, Kifurushi cha chini kabisa ni 120,000 kila mwezi, ni wachache sana wanaweza kumudu.
Airtel wameona fursa ya kulikamata soko kwa kudeal na gharama, kwa shilingi 110,000 unapewa router bure iliyoungwa bando la 110k kwa mwezi mzima na miezi ijayo unaweza kuunga kifurushi cha elf 70, 110k, 150k, n.k. Bando la elf 70 limekuwa kinara kwa gharama rafiki.
mitandao mingine wapunguze bei za vifurushi vya unlimited lasivyo watakuja kustuka Airtel kajitanua kawa Monopoly kameza soko