Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Huwa ni mara chache naunga mkono hatua za Magufuli lakini kwa hili la kununua ndege niliona kwamba ni mkakati ambao unaweza kuwa na manufaa kwa Tanzania. Nilikumbuka matatizo tuliyopata baada ya kuingia mkataba na South African Airways ambao walitukodishia ndege zao na tukapata hasara kubwa sana. Hata hivyo bado nina mashaka sana na uendeshaji wa Air Tanzania na menejimenti yake.
Watanzania wengi sana hupenda kuilinganisha Tanzania na Kenya, na kuona kwamba wanatuzidi sana, kuanzia mambo ya elimu, ushindani nafasi za kazi, na hata umahili wa shirika la taifa la ndege.
Sasa kuna tetesi kwamba Shirika la ndege la Kenya, katika ndege zote wanazotumia wao wanamiliki ndege tatu tu, na nyingine zote sio za kwao ni za mashirika na watu binafsi, kutia ndani vigogo wa Kenya. Na inaonekana kwa sasa Kenya Airways wana hali ngumu sana kifedha kutokana na kuendesha shirika kwa kutumia ndege za kukodi. Kwa hiyo ukilinganisha Tanzania na Kenya, kwa kuwa sisi tuna ndege za Air Tanzania tisa ambazo ni zetu wenyewe, tofauti na wao wenye kumiliki ndege tatu tu, sie tuko mbali sana na kuwazidi katika suala la shirika la ndege la taifa.
Kumbuka kwamba ukikodi ndege kama shirika la ndege, unailipia hata kama haifanyi safari, au inafanya safari kwa hasara. Hali ni tofauti kama unatumia ndege zako mwenyewe, unaweza hata kuzipaki mwezi mzima, kutegemea na hali ya biashara, bila kujali sana kwa kuwa ni zako.
Hali ngumu ya Kenya Airways imefanya hata kuwe na mpango wa kulikabidhi shirika hilo viwanja vyote vya ndege nchini humo viwe mali zake. Tetesi zinasema pendekezo hilo linatokana na wanasiasa vigogo wa Kenya ambao baadhi yao wanamiliki ndege za Kenya Airways, na baada ya kuona faida kubwa inayopatikana toka viwanja vya ndege, njia pekee ya kufaidika na faida hiyo ni kuvifanya viwanja hivyo vimilikiwe na Kenya Airways ambako wana shares. Wadau wazalendo wa Kenya wanapinga hatua hiyo, kwamba haileti maana kukabidhi viwanja vya ndege toka kampuni ya taifa ya Kenya Airport Authority (KAA) inayofanya kazi vizuri na kwa faida na kuviweka nchini ya Kenya Airways (KQ) ambao wanapata hasara kila mwaka. Hiyo ndiyo Kenya ya wenzetu.
Update on thread: Sio tetesi tena, source ni Daily Post ikiripoti jambo lililojadiliwa na Kamati ya Bunge
DAILY POST: SHOCK as it emerges KQ owns 3 planes only, 25 planes are owned by corrupt businessmen and State operatives - KINOTI please