SoC02 Aibu zetu, vilio vyetu

Stories of Change - 2022 Competition

Joannah

JF-Expert Member
May 8, 2020
20,240
47,273
Hapa napenda kuzungumza na kijana wa kitanzania aliyehitimu elimu ya juu na kuingia mtaani kusaka ajira.Kuna dhana moja iliyojengeka miongoni mwa vijana kwamba unapovua kofia yako kusherehekea ushindi ulioupata baada ya safari yako ya elimu basi huna budi kupata ajira rasmi kutoka serikalini au kwa asasi zisizo za kiserikali na sio kinyume na hapo.Mhitimu anapokosa ajira rasmi wengi wao wameshindwa kujikita kwenye kujiajiri binafsi hii ni kutokana na ugonjwa unatafuna jamii ya wasomi nao ni AIBU.Haka kaugonjwa kamezidi kuwa sugu kwenye jamii na kusababisha ongezeko la vilio vya ukosefu wa ajira kila kona ya nchi.Wacha nizungumzie Mimi binafsi nilivyoteswa na ugonjwa wa aibu na vile nimepambana nao.

Nilizaliwa katikati ya miaka ya 80,nilipata elimu yangu na kufanikiwa kumaliza kidato Cha sita kwenye moja shule za jeshi kwa ufaulu mzuri sana.Kwa vile nilisoma masomo ya sanaa wazazi wangu walinisisitizia sana nisomee sheria,sikuwahi kutamani hilo hivyo nikagoma,Nikaomba chuo,nikapata udahili kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam,nikachagua kozi ya sayansi ya siasa na masuala ya kijamii.

Mnamo mwaka 2011 nilihitimu elimu yangu ya juu,nikiwa binti mrembo kabisa mwenye ari na matumaini ya kupata ajira mara baada tu ya kuhitimu,nilikuwa napokea salamu za pongezi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki kwa mafanikio yangu,hakika nilijisikia vizuri ,nilijivunia Sana kuwa mdada msomi, hivyo imani yangu nilikuwa nikijua wazi nitapata ajira yangu muda mfupi tu.

Harakati za kusaka ajira zikaanza bila ya mafanikio. Nilisakanya pande zote za Tanzania lakini niliambulia patupu,Mara moja nilifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni fulani nikakataa eti mshahara mdogo!hakika kiwango changu cha kujiamini kilikuwa juu.Hatimaye mwaka ukakata nakula ugali wa shikamoo,mama wa kichaga kaanza kuwa mbogo anadai mimi na yeye mkataba wake ugali tu mambo ya kusuka nywele na vipodozi havimuhusu!Lawama zake Ni kwamba sikumsikiliza alivyonishauri nisome sheria,eti anaamini ningekuwa nimeshapata ajira ,kasahau kuna mamia ya wanasheria hawana ajira.

Mwaka wa pili baada ya kuhitimu nikaanza kufubaa,ule urembo nilikuwa nao kipindi cha chuo ukanaanza kuisha,si unajua tena tukiwa chuo tulivyo na mbwembwe kwa msaada wa bodi ya mikopo ,Sasa meza imepinduka!naanza kuishi Kama mkimbizi ndani ya nchi yangu ,naishi kwa kujifichaficha maana nimegubikwa na aibu sana.Nawaza kufanya biashara ndogondogo ila moyo unakataa kabisaa naona aibu sana msomi kama mimi kufanya vitu vidogo hivyo.Nikaendelee kula rumba nikilea gonjwa langu la aibu huku nikiendelea na kilio cha ukosefu wa ajira.Hamna sentensi inachoma roho kama ukutane na wahitimu wenzio halafu waulize "siku hizi uko wapi?usidhani wanakuuliza unapoishi,la hasha wanataka kujua umeajiriwa wapi,Basi unabaki kujiumauma tu.Kiukweli nilipigika Kama miaka miwili hadi nilipoamua kujitafakari hizi aibu zitanifikisha wapi mimi?ndipo nikafanya maamuzi.

MAAMUZI MAGUMU
Nikaamua nijiajiri,nikawaza vitu mbalimbali ambavyo ningeweza kujishughulisha navyo lakini nilibuma kwenye mtaji,kwa kuwa nilikuwa nachagua zile biashara za kisharobaro zenye kuhitaji maandalizi makubwa hivyo mahitaji ya pesa yanakuwa juu pia,Mara niwaze migahawa ya kisasa,Mara niwaze maduka ya kisasa ilhali mfukoni kwangu sina kitu,vichekesho!

Mwisho nikawaza kwa Nini nisiingie kwenye ushonaji?maana sio bei sana nikafanya maamuzi ya kujifunza ushonaji,Kuna fundi mzuri sana pale mtaani nikaongea nae akasema nimpe elfu ishirini na tano kwa mwezi akaahidi miezi sita inanitosha kujua. Basi nikazungumza na bi mkubwa akakubali kunipa hiyo pesa japo hakufurahishwa na hilo yeye anawaza tu niajiriwe Ila hakuwa na namna ikabidi tu anipe, nikaanza kujifunza ufundi pale kwa fundi Ngonyani Ila nilipitia changamoto sana maana usisahau ndio mtaa niliokulia wakina mama wakija wananiuliza wewe si umemaliza chuo mbona upo hapa tena?

Wee nasikia aibu hadi natamani kuacha Ila nikakaza moyo nikapiga pindi kwa miezi sita nikawa fundi stadi haswa vitu vichache Sana vilinishinda.Nikazungumza na bi mkubwa akanikopea vikoba laki tano nikapata cherehani,overlock,mikasi,nyuzi na jora la lining.Kuna chumba hapo nyumbani Kama stoo nikapanga hivyo vitu ikapendeza sasa kazi inaanza.Safari ya kutafuta wateja ikaanza walengwa wa kwanza Ni marafiki waliopo makazini,muitikio ilikuwa mkubwa sana kwa maana kila mmoja alikuwa akinifurahia na kunipa moyo nikashangaa hawa vipi?mbona kama wanaleta mizaha,maana mimi nashona Ila naamini nikiajiriwa ndio itakuwa sawa .

Nilifanya Ile kazi pale nyumbani ikaanza kukua,nikazidiwa na wateja pale nyumbani.Nikaweza kujiunga vikoba,nikacheza hata michezo kiufupi nikawa vizuri na Ile aibu ikaanza kuisha japo bado kale katamaa la kuajiriwa hakakuisha ndani yangu.Nikapata frame Sinza makaburini nikalipa nikaongeza mashine na Kaka msambaa wa kunisaidia Maisha yakaendelea.nikafanya kazi nikafanikiwa kununua kiwanja maeneo ya Mvuti japo palikuwa bado mashambani kipindi hicho.Nuru na matumaini vikarejea na malengo yakaanza kutimia. Cha kusikitisha Ile kiu ya kuajiriwa haikukoma mwenzenu.

HATIMAYE NAAJIRIWA RASMI
Mwezi wa kumi na mbili 2014 naitwa kwenye usahili,hiyo kazi niliomba siku za nyuma kidogo hata nilishasahau,nikafurahi kiana maana ni kampuni ya mabepari ambayo kwa macho ya nje jamii inahisi Kama wafanyakazi wake wanalipwa mamilioni na ndivyo pia nilidhani.Basi siku ya usahili nikafanya na nikaambiwa nitajulishwa,baada ya wiki mbili nikaitwa kazini.Wazazi walifurahi Ila wakaniuliza kuhusu ofisi yangu ya Sinza nikaahidi kuisimamia vizuri chini ya msaada wa kijana wangu msambaa.Basi nikaanza hiyo kazi kwa mshahara wa kawaida Ila wakiahidi kuniongezea kila ninapo ongeza mkataba.Nilifurahi nikaona haya ndio maisha Sasa Ila nikasema nitafanya yote mawili

Yaliyonikuta sasa hayakuwa madogo,Hiyo ofisi nikiingia asubuhi kutoka saa kumi na moja ,nipo hoi siwezi kwenda Sinza Kama nilivyodhani nitafanya hivyo narudi nyumbani,nikaanza poteza wateja wangu taratibu maana sipatikani kila wanaponihitaji. Hatimaye msambaa akaanza nihujumu anashona anakula mwenyewe pesa nikiuliza vipi anasema hakuna kazi,Natakiwa kulipa kodi kutoka mfukoni ofisi haijiendeshi,nikaona isiwe tabu baada ya miezi kumi toka niajiriwe nikafunga ofisi yangu.

Kule ofisini sasa,mambo yakawa sivyo hata nilikuwa nikifikiria,Kwanza mkataba mfupi hivyo kukosa hata sifa tu za kukopesheka kwenye taasisi za fedha, Ila pale ofisini wanatoa kamkopo fulani kasiko hata na tija ndio nikawa nakopa, mshahara haukutani jamani na mie kumbuka nilishazoea zile pesa za kila siku maisha yakawa kawaida mno, kuna Ile heshima tu kwamba anafanya kazi kampuni fulani.

Sikuzoe kuwa chini ya mtu anayeitwa bosi basi nikawa najionea mapichapicha tu,kwa kweli inahitaji uvumilivu kuwa chini ya mtu hasa ukishajua jinsi ya kuwa bosi wewe mwenyewe.Kuhusu kuongezewa huo mshahara jamani eti unaongezewa elfu ishirini walinimaliza nguvu sana,nikaona hapa sio mahali sahihi kwangu,Kuna mambo mawili natakiwa kufanya kati ya kuhama kampuni nitafute kazi nyingine au nirudie ofisi yangu ya Sinza, hapo Sasa nikawa nina mgogoro binafsi,sielewi nifanyaje.

Nikaanza kugusia kwa bi mkubwa nataka niache kazi nirudie biashara yangu,Uwiiii nilisemwa jamani akamshirikisha na mzee nilinangwa hadi nikawa mpoleee.Nikaendelea na hiyo kazi huku sina furaha maana nikiacha nitawaambia nini wazee wangu?sikutaka kuwapa msongo wa mawazo,maana wenyewe roho zao kwatu msomi wao kapata kazi yenye heshima.nikaendelea kupambana sikuwa na namna.

Miaka kadhaa ikapita,mwanzoni mwa mwaka 2020 kukazuka janga la Covid19,kukawa na wimbi la watu kupunguzwa kazi kwenye baadhi ya taasisi binafsi,Basi nikatumia fursa hiyo kutosaini mkataba mpya kwa hiari yangu.Pale ofisini kukatokea sintofahamu,kila mtu anatamani kujua kwa nini nimeamua hivyo nikawajibu nina masuala ya kifamilia natakiwa kuyashughulikia. Nilivyokamilisha taratibu zote mimi huyo kinyonge mpaka kwa wazee nikawaambia kilichotokea na sababu Ni Covid 19 .Hakika walisikitika Sana na kunipa moyo kwamba kila kitu kitakuwa sawa nikasikitika nao sana mpaka vimachozi vinalenga,Mambo ya ajira rasmi yakaishia hapo.

KURUDI UPYA MTAANI
Kwa kuwa nilikuwa nina vipesa fulani haikuwa ngumu kusimama tena,nilikodi frame nzuri maenea ya Tabata segerea nikaongeza mashine kubwa mbili nzuri ,nikatafuta fundi mzuri nikampata Mwakeye,Ni fundi hasa anadai alikuwa anashona DR Congo mishono migumuu ukilinganisha na mishono ya Tanzania Kazi ikaanza ,safari hii mambo yamekuwa tafrani yanakwenda ndivyo sivyo ,yaliyonikuta looh!mpaka nilijuta kuzaliwa ,hakuna rangi sijaacha kuona.Changamoto Ni kwamba sina wateja wa kutosha hivyo sina kipato,nikagundua sababu zifuatazo

1.Kubadilika kwa biashara,kipindi cha nyuma kulikuwa na mfumko wa kina mama na kina dada kushona nguo kwa mafundi wa nyumbani,Sasa mchina kaharibu soko nguo Ni tele madukani na bei ni rahisi hivyo wateja kukumbilia dukani

2.Kudorora kwa kipato miongoni mwa watanzania wengi

3.Biashara ya mtandaoni,ukiimarisha himaya yako ndivyo utavyopata wateja wengi na mimi ndio kwanza ndio nilikuwa najikongoja hivyo kukosa wateja wa kutosha

Kwa kweli changamoto zikanizidi nguvu,Mambo yakawa meusi mno ,kila ninachopanga hakiendi.Ile akiba kidogo niliyokuwa nayo imeisha nategemea ofisi ijiendeshe lakini hakuna kitu kinaendelea nadaiwa kodi,Mwakeye nae hanielewi anadai alipwe.Nikarudia ule mpauko wa siku zile baada ya chuo hakika nilipita kipindi kigumu. Hiki ndio kipindi nilipoteza watu wengi wa karibu nadhani mnafahamu vile watu hawapendi stori za matatizo.

Pia nilitamani nisikutane hata na mtu ninamjua haswa wa Ile ofisi niliyoacha kazi maana nilikuwa naona aibu sana.Baada ya joto kuzidi Mwakeye akaniaga anasafiri kidogo kumbe ndio kajiongeza,kaondoka! Nikabaki peke yangu naganga njaa pale huku nawaza njia za kujikomboa. Siku moja nimekaa pale ofisi ikapita gari ya shule nikaiangalia huku nawaza Mara wazo likanijia kwa nini nisitafute tenda mashuleni, nikaona hili Ni wazo la kufanyia kazi nikanunua vitambaa vizuri vya bei rahisi tu nikatengeneza sare nzuri tu Kisha nikafunga kwenye mifuko ya plastic nikatoa wiki mbili nitakuwa asubuhi napita mashuleni halafu ndio naenda ofisini.

Nikaanza kuzunguka shule tofauti bila mafanikio,shule ya tano wakavutiwa na kazi ni shule moja nzuri tu katika wilaya ya Ilala wakanipa masharti ya kuwaisha kazi wiki tatu kabla ya shule kufunguliwa kwa kuwa aliyepita amesumbua kwenye hicho kipengele, nikawahakikishia kuwahisha mzigo. Basi tukafanya taratibu zote za kukabidhiana kazi hawakuwa wababaifu baada ya wiki moja pesa ya awali yote ilishalipwa benki. Yaani sikuamin maana haikuwa pesa ndogo nikatafuta deiwaka watatu huwa wametega Tandika kuna chimbo la mafundi tukaanza kazi nachekelea mpaka jino la mwisho.Hapa ninavyoandika kwa kweli maisha yangu yapo vizuri,riziki inapatikana kuliko nilivyokuwa nimeajiriwa namshukuru sana Mungu.

HITIMISHO
Wadogo zangu mnaojiandaa kungia mtaani baada ya kuhitimu na mliopo mtaani tayari,jipeni Moyo na ujasiri mkuu.Hakikisha aibu haina nafasi kwenye harakati zako za utafutaji.Kuwa Kama umefungiwa kwenye chumba chenye giza totoro Ila unaahangaika kutafuta njia ya kutokea,endelea kupapasa mpaka upate upenyo .Kuendelea kulialia kuhusu ajira unaweza ukasubiri sana mwisho wa siku ukachelewa .Fanya chochote halali unachoweza pata riziki.

Pia tuachane na Ile dhana kwamba ukihitimu lazima uajiriwe ofisini ndio uwe bora,utapoteza muda Kama Mimi nilivyopoteza miaka yangu kadhaa kwa kuwa sikuwa na sababu ya kuacha kazi yangu kipindi kile naamini ningekuwa hatua nyingi mbele ya hapa nilipo,lakini nilikuwa na fikra finyu zikanipotezea dira.

Mwisho kabisa, kwa chochote utakachofanya zingatia Mambo haya.
1. Nidhamu, hii Iko kwa upana, kuwa na nidhamu ya muda,pesa na kwa watu unafanya nao kazi

2. Ubunifu, buni mbinu za kuboresha kazi yako.

3.Uchapakazi,

4.Mungu, mtangulize Mungu kwa kila jambo.
 
Hapa napenda kuzungumza na kijana wa kitanzania aliyehitimu elimu ya juu na kuingia mtaani kusaka ajira.Kuna dhana moja iliyojengeka miongoni mwa vijana kwamba unapovua kofia yako kusherehekea ushindi ulioupata baada ya safari yako ya elimu basi huna budi kupata ajira rasmi kutoka serikalini au kwa asasi zisizo za kiserikali,na sio kinyume na hapo.Mhitimu anapokosa ajira rasmi wengi wao wameshindwa kujikita kwenye kujiajiri binafsi hii ni kutokana na ugonjwa unatafuna jamii ya wasomi nao ni AIBU.Haka kaugonjwa kamezidi kuwa sugu kwenye jamii na kusababisha ongezeko la vilio vya ukosefu wa ajira kila kona ya nchi.Wacha nizungumzie Mimi binafsi nilivyoteswa na ugonjwa wa aibu na vile nimepambana nao.

Nilizaliwa katikati ya miaka ya 80,nilipata elimu yangu na kufanikiwa kumaliza kidato Cha sita kwenye moja shule za jeshi kwa ufaulu mzuri sana.Kwa vile nilisoma masomo ya sanaa wazazi wangu walinisisitizia sana nisomee sheria,sikuwahi kutamani hilo hivyo nikagoma,Nikaomba chuo,nikapata udahili kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam,nikachagua kozi ya sayansi ya siasa na masuala ya kijamii.

Mnamo mwaka 2011 nilihitimu elimu yangu ya juu,nikiwa binti mrembo kabisa mwenye ari na matumaini ya kupata ajira mara baada tu ya kuhitimu,nilikuwa napokea salamu za pongezi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki kwa mafanikio yangu,hakika nilijisikia vizuri ,nilijivunia Sana kuwa mdada msomi, hivyo imani yangu nilikuwa nikijua wazi nitapata ajira yangu muda mfupi tu.

Harakati za kusaka ajira zikaanza bila ya mafanikio. Nilisakanya pande zote za Tanzania lakini niliambulia patupu,Mara moja nilifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni fulani nikakataa eti mshahara mdogo!hakika kiwango changu cha kujiamini kilikuwa juu.Hatimaye mwaka ukakata nakula ugali wa shikamoo,mama wa kichaga kaanza kuwa mbogo anadai mimi na yeye mkataba wake ugali tu mambo ya kusuka nywele na vipodozi havimuhusu!Lawama zake Ni kwamba sikumsikiliza alivyonishauri nisome sheria,eti anaamini ningekuwa nimeshapata ajira ,kasahau kuna mamia ya wanasheria hawana ajira.

Mwaka wa pili baada ya kuhitimu nikaanza kufubaa,ule urembo nilikuwa nao kipindi cha chuo ukanaanza kuisha,si unajua tena tukiwa chuo tulivyo na mbwembwe kwa msaada wa bodi ya mikopo ,Sasa meza imepinduka!naanza kuishi Kama mkimbizi ndani ya nchi yangu ,naishi kwa kujifichaficha maana nimegubikwa na aibu sana.Nawaza kufanya biashara ndogondogo ila moyo unakataa kabisaa naona aibu sana msomi kama mimi kufanya vitu vidogo hivyo.Nikaendelee kula rumba nikilea gonjwa langu la aibu huku nikiendelea na kilio cha ukosefu wa ajira.Hamna sentensi inachoma roho kama ukutane na wahitimu wenzio halafu waulize "siku hizi uko wapi?usidhani wanakuuliza unapoishi,la hasha wanataka kujua umeajiriwa wapi,Basi unabaki kujiumauma tu.Kiukweli nilipigika Kama miaka miwili hadi nilipoamua kujitafakari hizi aibu zitanifikisha wapi mimi?ndipo nikafanya maamuzi.

MAAMUZI MAGUMU
Nikaamua nijiajiri,nikawaza vitu mbalimbali ambavyo ningeweza kujishughulisha navyo lakini nilibuma kwenye mtaji,kwa kuwa nilikuwa nachagua zile biashara za kisharobaro zenye kuhitaji maandalizi makubwa hivyo mahitaji ya pesa yanakuwa juu pia,Mara niwaze migahawa ya kisasa,Mara niwaze maduka ya kisasa ilhali mfukoni kwangu sina kitu,vichekesho!

Mwisho nikawaza kwa Nini nisiingie kwenye ushonaji?maana sio bei sana nikafanya maamuzi ya kujifunza ushonaji,Kuna fundi mzuri sana pale mtaani nikaongea nae akasema nimpe elfu ishirini na tano kwa mwezi akaahidi miezi sita inanitosha kujua. Basi nikazungumza na bi mkubwa akakubali kunipa hiyo pesa japo hakufurahishwa na hilo yeye anawaza tu niajiriwe Ila hakuwa na namna ikabidi tu anipe, nikaanza kujifunza ufundi pale kwa fundi Ngonyani Ila nilipitia changamoto sana maana usisahau ndio mtaa niliokulia wakina mama wakija wananiuliza wewe si umemaliza chuo mbona upo hapa tena?

Wee nasikia aibu hadi natamani kuacha Ila nikakaza moyo nikapiga pindi kwa miezi sita nikawa fundi stadi haswa vitu vichache Sana vilinishinda.Nikazungumza na bi mkubwa akanikopea vikoba laki tano nikapata cherehani,overlock,mikasi,nyuzi na jora la lining.Kuna chumba hapo nyumbani Kama stoo nikapanga hivyo vitu ikapendeza sasa kazi inaanza.Safari ya kutafuta wateja ikaanza walengwa wa kwanza Ni marafiki waliopo makazini,muitikio ilikuwa mkubwa sana kwa maana kila mmoja alikuwa akinifurahia na kunipa moyo nikashangaa hawa vipi?mbona kama wanaleta mizaha,maana mimi nashona Ila naamini nikiajiriwa ndio itakuwa sawa .

Nilifanya Ile kazi pale nyumbani ikaanza kukua,nikazidiwa na wateja pale nyumbani.Nikaweza kujiunga vikoba,nikacheza hata michezo kiufupi nikawa vizuri na Ile aibu ikaanza kuisha japo bado kale katamaa la kuajiriwa hakakuisha ndani yangu.Nikapata frame Sinza makaburini nikalipa nikaongeza mashine na Kaka msambaa wa kunisaidia Maisha yakaendelea.nikafanya kazi nikafanikiwa kununua kiwanja maeneo ya Mvuti japo palikuwa bado mashambani kipindi hicho.Nuru na matumaini vikarejea na malengo yakaanza kutimia. Cha kusikitisha Ile kiu ya kuajiriwa haikukoma mwenzenu.

HATIMAYE NAAJIRIWA RASMI
Mwezi wa kumi na mbili 2014 naitwa kwenye usahili,hiyo kazi niliomba siku za nyuma kidogo hata nilishasahau,nikafurahi kiana maana ni kampuni ya mabepari ambayo kwa macho ya nje jamii inahisi Kama wafanyakazi wake wanalipwa mamilioni na ndivyo pia nilidhani.Basi siku ya usahili nikafanya na nikaambiwa nitajulishwa,baada ya wiki mbili nikaitwa kazini.Wazazi walifurahi Ila wakaniuliza kuhusu ofisi yangu ya Sinza nikaahidi kuisimamia vizuri chini ya msaada wa kijana wangu msambaa.Basi nikaanza hiyo kazi kwa mshahara wa kawaida Ila wakiahidi kuniongezea kila ninapo ongeza mkataba.Nilifurahi nikaona haya ndio maisha Sasa Ila nikasema nitafanya yote mawili

Yaliyonikuta sasa hayakuwa madogo,Hiyo ofisi nikiingia asubuhi kutoka saa kumi na moja ,nipo hoi siwezi kwenda Sinza Kama nilivyodhani nitafanya hivyo narudi nyumbani,nikaanza poteza wateja wangu taratibu maana sipatikani kila wanaponihitaji. Hatimaye msambaa akaanza nihujumu anashona anakula mwenyewe pesa nikiuliza vipi anasema hakuna kazi,Natakiwa kulipa kodi kutoka mfukoni ofisi haijiendeshi,nikaona isiwe tabu baada ya miezi kumi toka niajiriwe nikafunga ofisi yangu.

Kule ofisini sasa,mambo yakawa sivyo hata nilikuwa nikifikiria,Kwanza mkataba mfupi hivyo kukosa hata sifa tu za kukopesheka kwenye taasisi za fedha,Ila pale ofisini wanatoa kamkopo fulani kasiko hata na tija ndio nikawa nakopa, mshahara haukutani jamani na mie kumbuka nilishazoea zile pesa za kila siku maisha yakawa kawaida mno,kuna Ile heshima tu kwamba anafanya kazi kampuni fulani.

Sikuzoe kuwa chini ya mtu anayeitwa bosi basi nikawa najionea mapichapicha tu,kwa kweli inahitaji uvumilivu kuwa chini ya mtu hasa ukishajua jinsi ya kuwa bosi wewe mwenyewe.Kuhusu kuongezewa huo mshahara jamani eti unaongezewa elfu ishirini walinimaliza nguvu sana,nikaona hapa sio mahali sahihi kwangu,Kuna mambo mawili natakiwa kufanya kati ya kuhama kampuni nitafute kazi nyingine au nirudie ofisi yangu ya Sinza,hapo Sasa nikawa nina mgogoro binafsi,sielewi nifanyaje.

Nikaanza kugusia kwa bi mkubwa nataka niache kazi nirudie biashara yangu,Uwiiii nilisemwa jamani akamshirikisha na mzee nilinangwa hadi nikawa mpoleee.Nikaendelea na hiyo kazi huku sina furaha maana nikiacha nitawaambia nini wazee wangu?sikutaka kuwapa msongo wa mawazo,maana wenyewe roho zao kwatu msomi wao kapata kazi yenye heshima.nikaendelea kupambana sikuwa na namna.

Miaka kadhaa ikapita,mwanzoni mwa mwaka 2020 kukazuka janga la Covid19,kukawa na wimbi la watu kupunguzwa kazi kwenye baadhi ya taasisi binafsi,Basi nikatumia fursa hiyo kutosaini mkataba mpya kwa hiari yangu.Pale ofisini kukatokea sintofahamu,kila mtu anatamani kujua kwa nini nimeamua hivyo nikawajibu nina masuala ya kifamilia natakiwa kuyashughulikia. Nilivyokamilisha taratibu zote mimi huyo kinyonge mpaka kwa wazee nikawaambia kilichotokea na sababu Ni Covid 19 .Hakika walisikitika Sana na kunipa moyo kwamba kila kitu kitakuwa sawa nikasikitika nao sana mpaka vimachozi vinalenga,Mambo ya ajira rasmi yakaishia hapo.

KURUDI UPYA MTAANI
Kwa kuwa nilikuwa nina vipesa fulani haikuwa ngumu kusimama tena,nilikodi frame nzuri maenea ya Tabata segerea nikaongeza mashine kubwa mbili nzuri ,nikatafuta fundi mzuri nikampata Mwakeye,Ni fundi hasa anadai alikuwa anashona DR Congo mishono migumuu ukilinganisha na mishono ya Tanzania Kazi ikaanza ,safari hii mambo yamekuwa tafrani yanakwenda ndivyo sivyo ,yaliyonikuta looh!mpaka nilijuta kuzaliwa ,hakuna rangi sijaacha kuona.Changamoto Ni kwamba sina wateja wa kutosha hivyo sina kipato,nikagundua sababu zifuatazo

1.Kubadilika kwa biashara,kipindi cha nyuma kulikuwa na mfumko wa kina mama na kina dada kushona nguo kwa mafundi wa nyumbani,Sasa mchina kaharibu soko nguo Ni tele madukani na bei ni rahisi hivyo wateja kukumbilia dukani

2.Kudorora kwa kipato miongoni mwa watanzania wengi

3.Biashara ya mtandaoni,ukiimarisha himaya yako ndivyo utavyopata wateja wengi na mimi ndio kwanza ndio nilikuwa najikongoja hivyo kukosa wateja wa kutosha

Kwa kweli changamoto zikanizidi nguvu,Mambo yakawa meusi mno ,kila ninachopanga hakiendi.Ile akiba kidogo niliyokuwa nayo imeisha nategemea ofisi ijiendeshe lakini hakuna kitu kinaendelea nadaiwa kodi,Mwakeye nae hanielewi anadai alipwe.Nikarudia ule mpauko wa siku zile baada ya chuo hakika nilipita kipindi kigumu. Hiki ndio kipindi nilipoteza watu wengi wa karibu nadhani mnafahamu vile watu hawapendi stori za matatizo.

Pia nilitamani nisikutane hata na mtu ninamjua haswa wa Ile ofisi niliyoacha kazi maana nilikuwa naona aibu sana.Baada ya joto kuzidi Mwakeye akaniaga anasafiri kidogo kumbe ndio kajiongeza,kaondoka! Nikabaki peke yangu naganga njaa pale huku nawaza njia za kujikomboa. Siku moja nimekaa pale ofisi ikapita gari ya shule nikaiangalia huku nawaza Mara wazo likanijia kwa nini nisitafute tenda mashuleni, nikaona hili Ni wazo la kufanyia kazi nikanunua vitambaa vizuri vya bei rahisi tu nikatengeneza sare nzuri tu Kisha nikafunga kwenye mifuko ya plastic nikatoa wiki mbili nitakuwa asubuhi napita mashuleni halafu ndio naenda ofisini.

Nikaanza kuzunguka shule tofauti bila mafanikio,shule ya tano wakavutiwa na kazi ni shule moja nzuri tu katika wilaya ya Ilala wakanipa masharti ya kuwaisha kazi wiki tatu kabla ya shule kufunguliwa kwa kuwa aliyepita amesumbua kwenye hicho kipengele, nikawahakikishia kuwahisha mzigo. Basi tukafanya taratibu zote za kukabidhiana kazi hawakuwa wababaifu baada ya wiki moja pesa ya awali yote ilishalipwa benki. Yaani sikuamin maana haikuwa pesa ndogo nikatafuta deiwaka watatu huwa wametega Tandika kuna chimbo la mafundi tukaanza kazi nachekelea mpaka jino la mwisho.Hapa ninavyoandika kwa kweli maisha yangu yapo vizuri,riziki inapatikana kuliko nilivyokuwa nimeajiriwa namshukuru sana Mungu.

HITIMISHO
Wadogo zangu mnaojiandaa kungia mtaani baada ya kuhitimu na mliopo mtaani tayari,jipeni Moyo na ujasiri mkuu.Hakikisha aibu haina nafasi kwenye harakati zako za utafutaji.Kuwa Kama umefungiwa kwenye chumba chenye giza totoro Ila unaahangaika kutafuta njia ya kutokea,endelea kupapasa mpaka upate upenyo .Kuendelea kulialia kuhusu ajira unaweza ukasubiri sana mwisho wa siku ukachelewa .Fanya chochote halali unachoweza pata riziki.

Pia tuachane na Ile dhana kwamba ukihitimu lazima uajiriwe ofisini ndio uwe bora,utapoteza muda Kama Mimi nilivyopoteza miaka yangu kadhaa kwa kuwa sikuwa na sababu ya kuacha kazi yangu kipindi kile naamini ningekuwa hatua nyingi mbele ya hapa nilipo,lakini nilikuwa na fikra finyu zikanipotezea dira.

Mwisho kabisa,kwa chochote utakachofanya zingatia Mambo haya.
1.Nidhamu, hii Iko kwa upana,kuwa na nidhamu ya muda,pesa na kwa watu unafanya nao kazi

2.Ubunifu, buni mbinu za kuboresha kazi yako.

3.Uchapakazi,

4.Mungu, mtangulize Mungu kwa kila jambo.
Asante sana kwa andiko zuri natamani kuandika yangu ila ni mvivu wa kuandika ila naamini kupitia wewe na historia yangu kuna kijana mmoja mtaani atasema bado hajashindwa atasimama

Thanks a lot Joannah
 
Nina matatizo mawili moja ni mvivu wa kuandika na pili nikianza kuandika uwa nafika kati najihisi kuumia sana kiasi cha kushindwa kumalizia sababu ni mapambano makali lakini iko siku nitashuka mkeka hapa
Pole Sana,kwani bado unapitia changamoto?mapito yetu tunayopitia yanaacha makovu mioyoni mwetu Mara nyingi makovu haya yamekuwa yakitukumbusha uchungu huo
 
Ajira ajira ajira...

Nlifungua mgahawa nikaufunga.

Biashara ya mafuta 😢

Mobile accessories.. + Movie Library 😢..

Mapambano bado yanaendelea ..

Hongera Sana Mkuu Vote yangu umepata .. kupitia andiko lako nimejifunza Kitu
Pambana pambana ndugu yangu!kitaeleweka tu Ni mwendo wa kukomaa tu .....nafurahi kusikia umejifunza kitu...Asante sana
 
Aibu yangu kilio changu,

Jinsi muonekano ,elimu, Viburi vinavyotunyima Mambo mazuri japo mambo hayo ni lazima yashushe hadhi zetu kwanza ndipo Tuone uzuri wake..
We be like ' The way im handsome, intelligent , Cute Mimi nifanye KAZI ile watanichukuliaje .. watanionaje .. esp pale unapokuwa ushatengeneza image flani hivi kwenye jamii as a deity , A man or a woman of no flaws ila deep down Unajua mwenyewe wewe ni nani na ni vita vingapi na vikali kiasi Gani unapambana .

On the run Maisha yanaenda hovyo , depression hii hapa , ule uangavu wa sura /mwonekano unaanza kupotea, nafsi inakusuta like till when buddy utaact unavyoact .. be a man , unaamua kuishi uhalisia , Unakiua kiburi na majivuno, weka vyeti ndani, tumia elimu uliyoipata kufanya maajabu ..

....... To be continued
 
Habari yako ndugu, Joannah.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo

Ahsante!!
Salama Kaka Deo....nitapita kusoma pasi na shaka
 
Aibu yangu kilio changu,

Jinsi muonekano ,elimu, Viburi vinavyotunyima Mambo mazuri japo mambo hayo ni lazima yashushe hadhi zetu kwanza ndipo Tuone uzuri wake..
We be like ' The way im handsome, intelligent , Cute Mimi nifanye KAZI ile watanichukuliaje .. watanionaje .. esp pale unapokuwa ushatengeneza image flani hivi kwenye jamii as a deity , A man or a woman of no flaws ila deep down Unajua mwenyewe wewe ni nani na ni vita vingapi na vikali kiasi Gani unapambana .

On the run Maisha yanaenda hovyo , depression hii hapa , ule uangavu wa sura /mwonekano unaanza kupotea, nafsi inakusuta like till when buddy utaact unavyoact .. be a man , unaamua kuishi uhalisia , Unakiua kiburi na majivuno, weka vyeti ndani, tumia elimu uliyoipata kufanya maajabu ..

....... To be continued
🙏Nasubiri mwendelezo tafadhali
 
Back
Top Bottom