NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,918
Kumbukumbu la Torati 22:5 >> Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
Tukiachana na kanisa hili la kilutheri kupasuka kila kukicha kwa migomo na vurugu kama ile vuta nikuvute ya mwaka jana Mbeya, nimeona pia kwenye suala la mavazi hawapo makini hata kidogo.
Leo katika kanisa la kkkt kijitonyama kumekuwa na wamama wanazunguka ndani ya kanisa kupinga uamuzi wa kuchomolewa kwa kiongozi flani, nguo walizovalia ni taiti na jeans zilizobana.
kanisa linawezaje kuwa la hovyo kiasi hiki kuruhusu waumini kujivalia wanavyotaka ?
Tuache ujinga wa kupotoshana kwamba sijui kinachoangaliwa ni roho mavazi hayapeleki mbinguni, Mungu alishaweka katazo kutokuvaa mavazi ya jinsia tofauti na pia mavazi ya kuvaa yawe ya kustiri, tunakoelekea kwa sasa zitaanzakvaliwa jeans zilizochanika (ripped jeans) kama hii ya kwenye picha.