Pre GE2025 Aibu kubwa kwa CCM. Propaganda yao ya Udini waliyotegemea kutackle Waraka wa TEC yafeli vibaya sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
17,046
36,498
Kwa ufupi ni kwamba CCM sasaivi imeishiwa mbinu za kuendelea kuwarubudi Watanzania na kuendelea kuwafanya Mazuzu.

Siku zinavyozidi kwenda, Watanzania wamezidi kuonyesha kuwa wameshawaelewa CCM kuwa ni wafitinishi, walaghai, waongo na Wasiolitakia mema hili Taifa zaidi ya kulinda matumbo yao.

Baada ya Kanisa Katoliki kusoma Waraka wake wa Pasaka ulioelekeza Wafungwa wa Kisiasa kuachiwa pamoja na Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi kabla ya Uchaguzi, CCM waliandaa mapandikizi yao na machawa wao kujaribu kuhamisha mjadala ili uonekane wa kidini na ili ionekane Kanisa Katoliki na Maaskofu wanamchukia Samia kwa sababu ni muislam.

Mungu si Athumani, propaganda hizi mfu walizokuja nazo CCM na vibaraka wao akiwemo Sheikh Mwaipopo aliyepo Mbeya zimekataliwa vibaya sana na Watanzania.

Watanzania kwa umoja wao wameonesha kukataa kurubuniwa na propaganda hizi za CCM na kusema kwa Wazi wamechoka dhuluma na Uonevu unaofanywa na CCM.

Watanzania kwa pamoja wameonekana wakihoji Mbona Kanisa Katoliki lilimsema na kumuonya Magufuli? ambaye alikuwa Mkristo na Mkatoliki mwenzao sasa udini wao upo wapi?

Watanzania wamehoji mbona Samia na vikosi vyake wamemuua Mzee Kibao ambaye ni muislam na hadi leo wapo kimya sasa udini wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki na wengineo upo wapi?

Nipende kuwapa polee sana CCM. Napenda kuwaambia kuwa nyakati hazirudi nyuma. Na ukomo wenu umefika hakika.

Mnaweza dhani kuwa nawatania ila kubalini tu tu Watanzania sasa hawawezi tena kurubuniwa na Propaganda zenu Mfu. Watanzania wanataka kuheshimiwa kwa Sanduku la Kura pamoja na Maamuzi yao kuwaweka Viongozi wanaowataka Madarakani.

Poleni sana CCM. Jueni mkiendelea kupambana na Maaskofu kifuatacho sasa ni kupambana na Wananchi direct then Jeshi la Wananchi.
Screenshot_20250420_095054_Chrome.jpg
 
Endelea kuota na kujipa matumaini feki.Wananchi wa Tanzania sio wajinga wa kuwafuata nyie na agenda zenu feki.Na wamewakataa na wataendelea kuwakataa.Na hapo huwa mnakuja na matusi kwamba sio waelewa.
Agenda zenu za maandamano zimekataliwa na zitaendelea kukataliwa.Ushahidi ni Mbowe alivyoitisha maandamano alishiriki yeye na binti yake.
Itisheni maandamano muone wangapi watajitokeza.Alibebwa Lisu kwenye mkutano na hakuna aliyemuunga mkono.
Endeleeni kuwa keyboard warriors na mashujaa wa mitandaoni.
 
Poleni sana. Kubalini tu kuwaachia wafungwa wa kisiasa na kuweka mifumo Wananchi wapate Viongozi wanaowachagua kweli ili muendelee kuishi kwa amani.

Mkiendelea kushupaza shingo hizo zitakatwa.
 
Mkuu kuna tatizo gani tukipata tume ya uchaguzi ambayo inatoa usawa na haki kwa kila chama.

Kuna tatizo gani tukipinga mauaji na utekaji holela unaofanya kisiasa?

Kuna ubaya?
 
Poleni sana. Kubalini tu kuwaachia wafungwa wa kisiasa na kuweka mifumo Wananchi wapate Viongozi wanaowachagua kweli ili muendelee kuishi kwa amani.

Mkiendelea kushupaza shingo hizo zitakatwa.
Mungu awape baraka wote wanaopaza sauti ya Haki na awalaani wasio ipenda sauti ya haki ila wanaipenda amani kwa dhuluma na nguvu za kimamlaka.
 
Acha waendelee kushupaza shingo. Siku itafika Wananchi wanaingia Mtaani alafu Jeshi litawaambia hatuwezi kupiga risasi Wananchi wasio na Hatia. It's Either mtoke au muwasikilize.
 
Endeleeni kuwa keyboard warriors na mashujaa wa mitandaoni.
Kwanza hakuna "keyboard warriors" huo ni msemo unaotumiwa na watawala madikteta na mafashisti uchwara.

Duniani kote hutumika vyombo vya kusambaza habari kuleta mabadiliko kwenye jamii. Zamani ilikuwa ni magazeti, Redio au taarifa za mtu kwa mtu.

Leo hii mitandao ya kijamii ndiyo nyenzo pekee ya haraka na inayodhibitiwa na jamii yenyewe, inayoweza kutumika kusambaza habari.

Sasa hao unaowaita "Keyboard warriors" unataka wafanye nini kuamini wanasaidia kuleta mabadiliko?

Wao wanatoa taarifa lakini kama jamii ya watanzania haigutuki wasilaumiwe wao!
 
Jamii haitaki hizo agenda zenu mnalazimisha.Keyboard warriors au Keyboard cowboys mnachochea na wananchi walio wengi hawawataki.Wananchi wakihitaji mabadiliko watayafanya.Nyie msijifanye mnawabebea akili na wakiwakataa mnawakashifu kwa matusi ya aina yote.
 
Back
Top Bottom