Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,550
MREMBO Betty Kitoo kama alivyojieleza, Alhamisi mchana wiki iliyopita alipatwa na aibu baada ya kukutwa akiwa mtupu kazini kwake. Kilichomfanya akae katika mazingira hayo kwa mujibu wa chanzo chetu ni tuhuma za kuvunja amri ya sita akiwa na mteja wake. Uwazi liliambiwa kuwa kazi aliyoajiriwa kuifanya mrembo huyo eneo la Kawe Ukwamani Jijini Dar es Salaam ni kutoa huduma ya masaji.
Awali chanzo kilidai kuwa mara nyingi Betty ametuhumiwa ‘kuchanganya madawa’ kwa kufanya kazi halali ya masaji aliyoajiriwa kuifanya sambamba na ‘kujiuza’ jambo ambalo limekuwa likiwakera wenzake.
HABARI ILIVYOVUJA
Waswahili hawakukosea kusema: “Kikulacho ki nguoni mwako.” Maana ndivyo ilivyokuwa kwa Betty kwani mvujisha soo alikuwa ni mmoja wa wafanyakazi wenzake ambaye hakupenda kazi ichanganywe na biashara ya ngono. “Sisi tunafanya kazi halali iliyosajiliwa, tunalipwa mishahara na tuna heshima kama wanawake.
“Lakini mwenzetu (Betty) ni kama hilo halizingatii, mteja akija akienda kumfanyia huduma ya masaji lazima amalizane naye. “Jambo hilo linatuvunjia heshima; wote tunaonekana kama makahaba tunaomba mtusaidie kukomesha hii tabia ya huyu msichana,” chanzo hicho kilidai.
USHAURI WATOLEWA
Kutokana na chanzo hicho kupiga simu chumba cha habari na kuomba Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kifanyie kazi ushauri ufuatao ulitolewa.
“Kwa maelezo yako jinsi yalivyo hauhitajiki uchunguzi mkubwa, wewe siku utakayoona huyo mwenzenu yuko kwenye dalili za kufanya uchafu wake wapigieni simu polisi. “Nitakupatia namba za polisi uwasiliane nao; siku ya tukio ukiwaambia polisi, utuambie na sisi kwa ajili ya kuja kuchukua habari.”
ZA MWIZI 40, MREMBO ANASWA
Kama wahenga walivyosema za mwizi 40 ndivyo ilivyomtokea Betty kwani haikuchukua zaidi ya siku 4 kunaswa tangu tuhuma dhidi yake zitolewe.
“Nimewasiliana na polisi yule uliyenipa namba zake amenipa namba za askari walioko doria nimeshawapigia. “Betty kapata mteja na kwa dalili ninazoziona atafanya machezo wake maana namuona kama kafuata kinga,” chanzo kilimwambia kiongozi wa OFM kwa njia ya simu jambo lililomfanya aandae mwandishi na mpiga picha kuwahi tukio tarajiwa.
OFM YAFIKA ENEO LA TUKIO
Haikuchukua muda mrefu kikosi kazi cha OFM kufika eneo la tukio ambako kilimkuta Betty akiwa chini ya ulinzi huku akiwa mtupu sambamba na mteja wake aliyetuhumiwa kuvunja naye amri ya sita. Hata hivyo mara baada ya kazi ya kupiga picha tukio hilo kuanza kwa kupata picha chache purukushani ilizuka kati ya OFM na polisi waliokuwa wakizuia mpigapicha wetu asipige picha tukio.
Sintofahamu hiyo kati ya waandishi wetu na polisi ilimpa mwanya mtuhumiwa wa kiume ambaye alikuwa amepagawa kutoka mbio eneo la tukio na kumwacha Betty akiwa mikononi mwa polisi.
MMILIKI WA OFISI AITWA
Baada ya Betty kunaswa na kuchukuliwa maelezo ya awali polisi aliuliza kuhusu mmiliki wa saluni hiyo ya masaji ambapo ilidaiwa kuwa amesafiri kwenda mkoani Morogoro. Aidha, polisi walipoomba namba za simu za mmiliki huyo walipozipiga hazikuweza kupatikana hewani.
MSAIDIZI WA BOSI AITWA
Baada kukosekana mmiliki huyo alipigiwa simu msaidizi wake ambaye alifika kwenye eneo la tukio ambapo alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo la aibu lililomkuta Betty alisema mrembo huyo alifanya uovu huo kivyake na siyo maagizo ya ofisi.
“Hapa kwenye ofisi yetu haturuhusu vitendo vya kufanya ngono tena ndani ya ofisi hilo ni kosa kubwa sana. “Huyu dada kitendo alichokifanya kimenisikitisha sasa sijui ni tamaa au ni kitu gani? Maana kwenye kazi hii bado mgeni pengine hilo ndilo lililomfanya akiuke maelekezo.
“Wenzake wanaofanyakazi hapa muda mrefu hatujawahi kuwasikia kufanya tabia hii mbaya,” alisema msadizi huyo bila kutaja jina lake. Baada ya mahojiano hayo mafupi kufanywa, polisi waliondoka na msaidizi huyo wa saluni na Betty ambaye ni mtuhumiwa wakidaiwa kupelekwa kituo cha polisi ambacho hakikufahamika ni cha wapi.