Munch wa annabelletz47
JF-Expert Member
- Aug 13, 2019
- 1,737
- 2,829
Mahakama ya Mkoa wa Tabora, imemuhukumu Kwenda jela miaka minne Juma Edward (30), Mkazi wa kijiji cha Shitage wilayani Uyui mkoani humo kwa kumuuwa mkewe Kulwa Vincent (29) kwa kumshambulia hadi kufa baada ya kumfumania akifanya ngono na mwanaume mwingine ambae ni jirani yao nyumbani kwake.
Akitoa adhabu hiyo leo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora Jovith Kato, amesema kwamba katika shitaka hilo mwanamke alijitakia mwenyewe kwa kukutwa akiwa na mwanaume mwingine ambaye sio mume wake ni jirani yao, na wamekuwa wakifanya hivyo zaidi ya mara mbili.
Hakimu huyo amesema kwamba Mahakama hiyo imeona impunguzie adhabu hiyo kutoka kifungo cha maisha hadi miaka minne kwa sababu aliweza kukubali shitaka lake na hakuisumbua mahakama kwamba alikiri kufanya mauaji hayo.
Kato katika hukumu hiyo alisema kwamba mshitakiwa alikuwa gerezani kwa muda wa miaka7, hivyo Mahakama ina jicho la huruma kutokana na kukaa kwake na kukiri shitaka lake lililokuwa likimkabiri la mauaji ya bila kukusudia kupitia kifungu cha sheria cha 195 na cha 198 ambacho ndio kilitumika dhidi yake.
Hapo awali mshitakiwa katika Mahakama hiyo aliweza kukiri kufanya mauaji na hakuweza kuisumbua Mahakama hiyo ndio maana imemuonea huruma kutokana na kuwa na uchungu baada ya kumfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine ambae ni jirani yao katika kitanda chake.
Mshitakiwa Juma Edward alikiri kufanya mauaji ya mke wake kutokana alikuwa na hasira lakini hakujua kama kitatokea kifo alijua anamuonya tu na sio kumuuwa.