Ahoua Jean Charles usajili bora zaidi Tanzania

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
923
1,616
Sio sababu ni MVP Ivory Coast pekee. Hapana. Hadi sasa tumeshuhudia wachezaji bora Ivory Coast wanatua katika ardhi Yetu. Aziz Ki na Pacome huwezi acha kuwataja - moja ya sajili bora kabisa katika ardhi zetu.

Hakuna anayepinga Aziz Ki na Pacome ni wachezaji bora katika league yetu. Sasa jaribu kufikiri huu ubora waliokua nao wangekua ni chini ya miaka 23 au hata 25? Sidhani kama ingekuwa ni rahisi kuwapata au kuwalinda katika league yetu. Lakini hao niliowataja tunaweza kuwapata au kuwalinda sababu tayari ni jioni. Jioni kwa maana ya kuwa ukiwa above 26 ni ngumu sana kucheza nje ya Africa.

Pia tunakubaliana kuwa West Africa ndio feeder wazuri wa League 2 -League 1 (France) pia kidogo North Africa. Hivyo basi wachezaji wadogo wengi wenye vipaji vikubwa huwa tunategemea basi safari yao ni League 2 au wameshindwa sana basi ni North Africa.

Leo Simba inaenda kumtambulisha MVP wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 katika ardhi ya Tanzania. Hili sio jambo dogo hata kidogo. Wengi watachukua jambo la kawaida, ila kiuhalisia ni jambo kubwa sana.

Wengi watasema labda ni garasa, hajui mpira. Nitaomba huyo mtu anitajie ni mwaka gani League 1- Ivory Coast ilizalisha MVP mwenye kiwango cha kawaida? Tofauti, na nchi nyingine, ile league haina ushindani kama maana ubora katika ramani ya soka Africa, ila ni ardhi yenye vipaji vikubwa sana.

Kufuatia kile nilichokieleza basi bila kigugumizi, natamka kuwa huu ndio usajili bora kwa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.

PIA SOMA
- Simba Sc tumemsajili kiungo wa Ivory Coast Ahoua Jean
 
Hadi sasa kawa ni moja ya wachezaji bora kuwahi kupita katika ardhi yetu katika miaka ya hivi karibuni:

Clatous Chama
Luis Miquissone(1st Move to Simba)
Morrison (1st move to Yanga)
Aziz ki
Pacome
Sakho
Kipre
Diarra.

Hawa nitawataja kwa heshima.

Emmanuel Okwi
Nonda Shabani
Patrick Mafisango
Haruna Nyonzima(1st move to Yanga)
Hamis Tambwe
Kipre Tcheche

Nitamalizia kwa kuwataja:

Fiston Mayele
Meddie Kagere ya
 
Sajili za makolo huwa ni za mihemko tu ngoja ngoma ianze tutayaona yale yale ya kina Fred na Jobe!

Nafasi ya tatu ndio inapendeza zaidi kolokoloni kwasasa!
 
Kremooo mlisema hivyohivyooo dhambiyake haitwaachaa
 
Sakho alikua na mchachari ila hana hatari kivile
 
Comments reserved
 
Ila safari hii nawaona kama simba wako serious eti!! Au mtani wangu Kalpana nasema uongo! Msimu huu naona kama hamtaki kabisa utani.

Sijui ni kwa sababu msimu uliomalizika mlishika nafasi ya 3! Au ni kwa sababu Boss mwenyewe amerudi kundini?
Hizo sababu ya kushika nafasi ya tatu na mashabiki kuja juu wamechoka longolongo.
 
Bila Yao Yao list ni batili.
 
Ila safari hii nawaona kama simba wako serious eti!! Au mtani wangu Kalpana nasema uongo! Msimu huu naona kama hamtaki kabisa utani.

Sijui ni kwa sababu msimu uliomalizika mlishika nafasi ya 3! Au ni kwa sababu Boss mwenyewe amerudi kundini?
Sio uongo mtani...kama na ww umeliona hilo basi kimenuka.... πŸ˜† πŸ˜† πŸ˜† 🀣 🀣 🀣 🀣 Tate Mkuu
 
Ila safari hii nawaona kama simba wako serious eti!! Au mtani wangu Kalpana nasema uongo! Msimu huu naona kama hamtaki kabisa utani.

Sijui ni kwa sababu msimu uliomalizika mlishika nafasi ya 3! Au ni kwa sababu Boss mwenyewe amerudi kundini?
Kwa kile tulichopitia msimu uliopita ilikua shule kubwa sana Mkuu . Tumeishi kwa mateso sana.

Tumejifunza(The hard way).
 
Usajili wa panic huu. Unaweza uka click au wakaanza wasimanga tena Mo na Mangungu wake.
Naona wengi mnatumuia neno panic, ila ndio msimu ambao simba wamesajili vizuri zaidi katika misimu ya hivi karibuni.

Kwa tafsiri yako yoyote ya panic, kama hii panic inafanya club isajili vizuri hivi, basi naomba iendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…