AHADI ZISIZOTEKELEZEKA JIMBO LA MOSHI MJINI KITANZI KWA CCM

mwanachuo

Member
Jan 15, 2013
40
36
Mwandishi wetu.
Wakati chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Mjini kikijinasibu kupitia Mbunge wa Chama hicho Jimbo la Moshi Mjini kuwa waliahidi ahadi 10 ambapo wanadai 9 zimekamilika na moja ya kuifanya Moshi kuwa Jiji kwamba ndiyo pekee imebakiwa, Chama hicho kimepata upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi kupitia Mbunge wao na kudai ni uongo tena usiovumilika.
Wananchi hao wanasema ikiwa chama hakita simama na kuwa walazimisha wabunge na madiwani wake ambao wameahidi ahadi nyingi kwenye jamii bila kuzitekeleza kitakuwa kimejichimbia kaburi.
Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema, Mbunge wa Moshi Mjini ameahidi fedha nyingi kwenye maeneo mbalimbali ambapo ameshindwa kabisa kutimiza, akisisitiza kuwa Viongozi wa Taasisi za dini, mashirika na vikundi mbalimbali vya kijamii vina mdai hizo ahadi ambazo alitoa kwa hiari yake.
Naye mwananchi mwingine aliyetamburika kwa jina moja la Mwajuma alisema, kibaya zaidi akipigiwa simu hapokei na akigundua ni wewe unaye mkumbusha deni anakublock.
Baada ya malalamiko haya, Msemakweli ilifanya jitihada za kumtafuta lakini simu yake iliita tu bila kupokelewa. Hata hivyo Msema kweli ilifika kwenye Taasisi za dini na vikundi kadhaa ambavyo vilitajwa kumlalamikia ambapo ilikutana na mambo mazito juu ya Mbunge huyu wa Jimbo la Moshi Mjini.
Msema kweli ilishangazwa na ushahidi uliotolewa wa ahadi kemkem ambazo kiujumla zinafikia mil 106 alizoahidi yeye Binafsi na nyingine kumtuma Katibu wake Mndeme.
Miongoni mwa ahadi hizo ni pamoja na ujenzi KCMC, Makanisa ya SDA, KKKT sharika tofauti tofauti, Hospital ya Mawenzi, St. Joseph, Msikiti mbalimbali ikiwemo Pasua, Kaloleni, ukarabati wa shule, ofisi za chama na vituo vya watu wenye mahitaji maalumu.
Katika vikundi, ameahidi zaidi ya vikundi 15 katika Kata mbalimbali ambavyo pia wamekiri kuchoka kumtafuta alipe.
Kutokana na Hali hiyo tulijaribu kuongea na Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM ambaye alisema tabia hii ya kuahidi na kushindwa kutekeleza inafanyika sana Moshi na Mbunge na baadhi ya Madiwani Hali inayokipaka chama madoa na kuahidi kupitia vikao vya chama Mkoa kuwasilisha madai hayo ili chama kitoe maelekezo kwenye Wilaya.
Msemakweli inaona Kuna haja ya Chama hiki kuchukua hatua za kinidhamu kwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi na kushindwa kutimiza kwani matendo yao yanahatarisha ustawi wa chama kwenye Kila ngazi.
Niliwasiliana na kada mmoja wa siku nyingi wa CCM Moshi ambaye alisema Hali sio shwari kabisa kwani mbali na Mbunge huyo kushindwa kuliongoza Jimbo, kwa kushirikiana na kiongozi mmoja wa chama ngazi ya Mkoa wameajiri vijana kwa ajili ya kutukana na kuchafua watu ambao wanaonekana wanajichanganya na jamii. Alisema vijana hao ambao wameahidiwa fedha na kupewa computer mpakato kutoka kwa kigogo mmoja anayefanya shughuli zake Zanzibar wameanzisha group la Whatsapp la Moshi ya Moto ambalo kazi yake kubwa ni kumtukana Ibraline, Meya wa Moshi ndugu Zuberi Kidumo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi. Vijana hao ambao hutumia namba bandia kuchafua watu ni pamoja na Idirisa Makishe mgonjwa wa cancer ambaye kutokana na Hali yake amejikipua hadharani kwa kutukana watu bila kupepesa macho, mwingine ni Hugo Tillya ambaye alikimbia nchini baada ya kuhusishwa na vitendo vya Ushoga ambaye ndiye mwanzilishi wa kundi Hilo, wengine ni vijana wa njoro, na pasua ambao hulipwa kati ya 100,000- 250,000 Kila mwezi kwa Sharti la kutukana post 10 Kila siku. Mara kadhaa Mbunge huyo amekuwa akiwatumia vijana hao kushughurikia wakosoaji wake badala ya kukamilisha ahadi alizo ahidi.
Ahadi ni deni na Dawa ya Deni kulipa.
 
Hiyo ni vita ya makada wa CCM, haina faida yoyote kwa wananchi wa kawaida.
Moshi kimaendeleo ilishakufa na kuzikwa na CCM. Hakuna tena mwamko wa kimaendeleo, usafi au usalama uliokuwepo siku za nyuma. Kwa sasa, kwenye kukuza uchafu nadhani Manispaa ya Moshi ni Kinara. Tangu 2020 CCM imeigeuza Moshi kuwa kimji kidogo kilichojaa walevi na mashoga.

CCM ni laana.
 
Hiyo ni vita ya makada wa CCM, haina faida yoyote kwa wananchi wa kawaida.
Moshi kimaendeleo ilishakufa na kuzikwa na CCM. Hakuna tena mwamko wa kimaendeleo, usafi au usalama uliokuwepo siku za nyuma. Kwa sasa, kwenye kukuza uchafu nadhani Manispaa ya Moshi ni Kinara. Tangu 2020 CCM imeigeuza Moshi kuwa kimji kidogo kilichojaa walevi na mashoga.

CCM ni laana.
moshi was doing good until alipokuja yule mtu wa niletee fulani. Akawaletea viongoz wasion na uwezo wowote hapo moshi
 
Hiyo ni vita ya makada wa CCM, haina faida yoyote kwa wananchi wa kawaida.
Moshi kimaendeleo ilishakufa na kuzikwa na CCM. Hakuna tena mwamko wa kimaendeleo, usafi au usalama uliokuwepo siku za nyuma. Kwa sasa, kwenye kukuza uchafu nadhani Manispaa ya Moshi ni Kinara. Tangu 2020 CCM imeigeuza Moshi kuwa kimji kidogo kilichojaa walevi na mashoga.

CCM ni laana.
Kiukweli katika miji inayochakaa kwa kasi ni pamoja Moshi, ulevi , uchafu na ujenzi holela vimeshika kasi
 
Back
Top Bottom