Kastori Kalito
Member
- Jul 31, 2022
- 17
- 13
Kilimo-Utalii ni aina ya utalii unaojumuisha shughuli za kilimo, ambapo wageni husafiri kwenda maeneo yaliyopangiliwa vema ili kupata uzoefu unaohusiana na kilimo na maisha ya vijijini na mijini. Aina hii ya utalii inalenga kutoa uzoefu wa vitendo na kielimu kuhusu kilimo, desturi, na mazingira ya asili. Kilimo-Utalii ni wazo bunifu linalolenga kupanua vyanzo vya mapato kwa serikali za mitaa na kitaifa, kutoa fursa za ajira endelevu kwa vijana, kudumisha tamaduni na maadili, na usalama wa chakula.
Kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania kwa miongo kadhaa. Mfano, kwa mujibu wa Ripoti ya Uchumi 2020, kilimo kilichangia asilimia 26.5 ya pato la taifa, na uzalishaji wa mazao na mifugo kuchangia kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, sekta hii inajumuisha wakulima wengi wadogo wanaotegemea mbinu za jadi.
Kilimo-Utalii kinaweza kuwa sehemu ya wakulima kupata uzoefu wa kipekee na kuchochea kilimo endelevu. Vituo vya Kilimo-Utalii vinaweza kuwa sehemu ya kujifunzia ambapo makundi ya wanafunzi, watafiti, na wapenda kilimo wanaweza kupata maarifa ya vitendo kuhusu kilimo.
MFANO WA MUONEKANO WA VITUO/MASHAMBA YA KILIMO-UTALI KWA MKUTADHA WA VIJIJINI;
Mandhari Asilia. Matumizi ya vifaa vya kienyeji kama vile mbao, majani, na udongo katika ujenzi vitasaidia kuunganisha wageni na mazingira ya asili.
Nyumba za Wageni. Katika mitindo ya jadi na vifaa vya kisasa imara.
Bustani za Mimea. Bustani zenye mimea ya asili na ya tiba, pamoja na vitaluu vya mimea mbalimbali.
Maji. Mabwawa, vijito, na sehemu za umwagiliaji zinazoweza pia kuwa maeneo ya burudani kama vile uvuvi na kutazama ndege.
Shughuri za Kijamii na Kitamaduni. Maeneo ya kufanyia shughuli za kitamaduni kama ngoma, hadithi za jadi, na michezo ya asili.
MUONEKANO WA VITUO/MASHAMBA YA KILIMOUTALI MIJINI.
Muonekano wa Kisasa. Vitu/mashamba ya mijini yenye muonekano wa kisasa huku vikihifadhi baadhi ya vipengele vya kijijini. Matumizi ya vifaa vya kisasa kama viooo, vyuma, na saruji, lakini na mpangilio unaolenga kijani na uzuri wa asili.
Mazingira ya Kilimo ya Mjini. Mashamba ya mijini kama vile bustani za paa, kilimo cha wima na Mazingira yenye mpangilio mzuri na rahisi kufikika.
BIDHAA/HUDUMA ZA KILIOMO-UTALII (AGRO-TOURISM PRODUCTS/SERVICES
Hizi shughuli zinaweza kufanyika katika maeneo maalumu, yaliyoundwa kwa ustadi na ubunifu, mijini na vijijini, hivyo kutoa uzoefu kamili wa kilimo, kutoka kwa mila za jadi hadi kilimo mijini.
MBINU ZA KUENDELEZA NA KUFANYA WAZO HILI KUWA HALISI
i. Mpangilio na Tathmini. Kuainisha na Kutenga maeneo maalum katika kila mkoa. Mfano, awamu ya kwanza inaweza kuhusisha idadi kadhaa ya mikoa, kama vile mikoa mitano kwa miaka mitano ya mwanzo ambapo vituo vya Kilimo-Utalii vinaweza kujengwa, na kuongeza mikoa mingine kila baada ya miaka mitano hadi kufikia mikoa 25 kwa miaka 25. Kuzingatia sifa za kipekee za kilimo kama vile mifumo ya kilimo ya kisasa na asilia, njia za umwagiliaji za jadi kwa kutumia mito, mabwawa, mifereji, na visima vya kudumu, na mbinu za kilimo endelevu. kubuni uzoefu wa kipekee wa wageni/watalii kufurahia,kutangaza vituo vya Kilimo-Utalii kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano kama mitandao ya kijamii n.k
ii. Skeli za Utekelezaji wa Wazo Hili.
Wazo la Kilimo-Utalii linaweza kuwa halisia kwa mtu binafsi, kikundi cha watu au taasisi za serikali/serikali kuu. Watu binafsi wanaweza kuanzisha vituo vya Kilimo-Utalii kwa kutumia rasilimali walizo nazo kama ardhi na shughuli za kilimo. Kikundi cha watu, kwa mfano wakulima au wahitimu kutoka vyuoni ama, vikundi vya wanawake, wanaweza kuunda ushirika na kufanya mipango shirikishi ili kuanzisha vituo vya Kilimo-Utalii, Taasisi za serikali kama wizara ya Kilimo/serikali kuu zinaweza kuunda sera rafiki na kuja na mkakati mkubwa wa kuanzisha vituo vya KilimoUtalii katika mashamba ya serikali kama ile mashamba ya chai, na kahawa au kwa kuanzisha mashamba/vituo maalumu vya KilimoUtalii pekee.
iii. Uuzaji na Uhamasishaji [Marketing and Promotion]
Kampeni ya kukuza Kilimo-Utalii kitaifa, Kikanda na kimataifa. Kutumia mitandao ya kijamii, Radio na Televisheni.
iv. Mbinu Endelevu (Sustainable Practices).
Kutekeleza mbinu za kilimo rafiki kwa mazingira na juhudi za uhifadhi. Kupigia debe kilimo cha kikaboni, kupunguza taka, na matumizi ya nishati mbadala.
FAIDA ZA MUDA MREFU ZA KILIMO-UTALII
a) Ukuaji wa Kiuchumi.
Kuchochea mapato thabiti kwa jamii za vijijini na mijini. Kukuza uchumi wa eneo kwa kuvutia watalii na kusaidia biashara ndogo ndogo.
b) Uhifadhi wa Utamaduni
Kuhamasisha uhifadhi na kuendeleza mbinu za kilimo na maisha ya vijijini. Kukuza fahari na ufahamu wa utamaduni kwa wanajamii na watalii
c) Maendeleo Endelevu
Kukuza mbinu za kilimo endelevu na utunzaji wa mazingira. Kusaidia uhifadhi wa rasilimali asili na bioanuwai.
d) Fursa za Elimu na Burudani.
Fursa za kujifunza kwa vitendo kuhusu kilimo, uendelevu, na maisha ya vijijini. Kutoa shughuli za burudani zinazowakutanisha watu na asili na utamaduni wa eneo husika..
Kilimo-Utalii sio tu njia ya kukuza uchumi bali pia ni chombo cha kurejesha kilimo kama uti wa mgongo kwa jamii kubwa yenye rasilimali duni, kuchochea maendeleo ya jamii za vijijini, kutoa ustawi na kupunguza msongo wa mawazo kwa jamii, na kuhifadhi urithi wa kitamaduni. Kilimo-Utalii kinaweza kuunda mustakabali endelevu na wenye mafanikio kwa Tanzania.

- Makazi ya shambani(farm stays)
- Shughuri za kujichumia matunda/mboga mboga
- Ziara za mashambani(farm tours)
- Warsha za elimu( educational workshops)
- Mikahawa ya chakula cha shambani/jadi chenye virutubisho asilia
- Sherehe za mavuno
- Mwingiliano na wanyama
- Masoko ya kazi za mikono za kisanaa kama vile vinyago n.k,
- Fursa za wageni/watalii kufanya ziara za vyakula vya asili
- Vituo/mashamba ya Kilimo-Utalii kama bank za kuhifanyi/ kutunza mimea asilia/tiba, rasilimali za kijenetikia za mazao/mbegu, na utalii wa kimazingira. Kila moja ya huduma hizi itachangia kwa njia yake kukuza uchumi wa eneo, kuhifadhi utamaduni, na kutoa fursa za elimu na burudani.