SoC04 Afya ya akili Kwa Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Depearl

New Member
Jun 10, 2024
1
2
AFYA YA AKILI KWA TANZANIA TUITAKAYO
What-different-types-of-counselling-are-there.jpg


Kama ilivyo muhimu Kwa nyanja nyingine za afya ndivyo Afya ya akili Kwa Kila mtanzania itainua ubora wa afya ya jamii Kwa watoto, vijana na wazee. Je,afya ya akili ni mpaka iwe tatizo la akili,la hasha Afya ya akili ni mchepuo wa kisaikologia unaohusisha uboreshaji wa fikra za kibinadamu pamoja na tabia yake Ili kukabiriana na hali tofauti tofauti za kimazingira . Kwahiyo Kila mwanadamu anapitia changamoto ya akili Kwa viwango vya kawaida au kiasi na viwango hatari au kukithiri.

Tanzania imeweza kufanya jitihada tofauti tofauti za kueneza mambo yahusuyo afya ya akili,kupitia asasi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali. Tanzania Psychological Association ikiwa moja ya asasi hizo,inayosimamia afya ya akili ,lakini bado hatujafikia malengo sitahiki kama watanzania kuhusu afya ya akili hivyo mapendekezo yafuatayo yanaweza kufikisha mahali pazuri ndani ya miaka 5 Hadi 25.

Uwekezaji katika uvumbuzi na uchambuzi juu saikolojia itayohusisha Elimu kwanzia shule za msingi Hadi vyuo vikuu. Kwasasa vyuo vinavyotoa elimu ya saikolojia ni vichache kuzingatia uhitaji wa huduma za afya ya akili nchini . Ikiwemo kutoa nafasi za kupata ujuzi wenye hadhi ya kimataifa juu ya swala la Afya ya akili,itakayopatikana hapa hapa nchini.

Utolewaji wa huduma za afya ya akili katika hospitali za kata na wilaya pamoja na kliniki nyingine zianzishwe na kueneza huduma hii isibaki kwenye hospitali kubwa pekee. Ili kusaidia na watu wa vijijini ambao Kwa asilimia kubwa hawajui hata kuhusu afya ya akili.

Kuanzisha na kuboresha maabara zitakazotumika katika kuratibu huduma za afya ya akili kama vile kitaalamu maabara za Cognitive Psychology, Clinical psychology na neurology laboratories. Ili kuwezesha kufanyika Kwa chunguzi muhimu za sayansi ya saikolojia na kuboresha afya ya akili nchini Kwa viwango vya kimataifa.
Kuanzisha Sheria muhimu ambayo itadhibitisha Bima ya Afya kutumika kutoa huduma ya Afya ya akili nchini Kwa Kila mtanzania Kwa gharama nafuu,Ili kusaidia mtanzania wa hali ya chini kupata huduma za afya ya akili Kwa urahisi na uharaka.

Kutoa leseni halali Kwa wanasaikologia waliosomea na kufuzu Kwa uweledi kada hii,Ili kuepusha walanguaji wanatoa huduma za afya ya akili nchini kiholela na kusababisha madhara zaidi Kwa watanzania.
Kuweka uhusiano wenye tija kati ya madaktari na wanasaikologia katika kushirikiana Kwa pamoja kusaidiana kutoa huduma hii kwasababu utoaji wa Afya ya akili unategemea kiwango Cha magonjwa mengine shirikishi yatokanayo na magonjwa ya akili. Kwahiyo kama inatolewa Kwa mtu mwenye changamoto ya akili hatari au iliyokithiri dawa zinaweza kuhusishwa.

Kutokomeza vichochezi vya matatizo ya Afya ya akili nchini ikiwemo umasikini,ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya Afya ya akili na upotoshaji utokanao na mila kandamizi ambazo Zinapotosha juu ya changamoto ya akili na kuzuia watu kuelimika juu ya swala la Afya ya akili nchini.

Ikumbukwe kwamba Afya ya akili sio ugonjwa ila ni changamoto,na inaweza kutolewa Kwa mtu wa kawaida au mwenye changamoto ya akili hatari kama vile sonona. Pia huduma za unasihi kama counseling na psychotherapy ni muhimu Kwa utulivu wa akili ya binadamu."AFYA YA AKILI,UBORA NA USALAMA WA JAMII"
 
Back
Top Bottom