.., sisi vijana tumekumbwa na kitu gani nyakati hizi!?
Humphreys Polepole mwaka 2014/2015 alikuwa mstari wa mbele sana kupambana kupata mabadiliko ya katiba mpya.., na alipambana haswaa, hadi tume ya Mabadiliko ya katiba kuundwa, yeye (Polepole) akiwa ni mjumbe wa Tume hiyo..
Jana wakati akiwa kwenye kipindi cha 'Kikaangoni' cha EATV, anaulizwa swali, vipi kuhusu upatikanaji wa katiba mpya, anajibu kwa njia rahisi sana, eti "HILO MNIACHIE KWENYE KAPU LANGU.., SASA MTUACHE KWANZA TUINYOOSHE NCHI"..., Polepole leo anasema 'Katiba mpya hakuna, wanainyoosha nchi!!? Daah!
Kweli nimeamini.., kila mtu ni mbinafsi, haswa pale anapotimiza matakwa yake.., kila mtanzania ni mbinafsi kwa wakati wake (na ndiyo maana wale wanafunzi wa elimu ya juu waliopata mikopo wao hawa-hoji tena kuhusu wenzao wenye sifa waliokosa mikopo hiyo, wamenyamaza kimya!!!)
Afrika; ni dhambi sana, kubwa sana, kuongea wakati wa kula.., ni kufunga mdomo wako na kula bila kutoa sauti..,