Afrika Kusini: Kesi ya ufisadi ya Zuma yaahirishwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,127
1,929
Kesi ya ufisadi nchini Afrika Kusini inayomkabili Rais wa zamani Jacob Zuma imeahirishwa tena kusubiri matokeo ya rufaa ya kiongozi huyo wa zamani ya kutaka mwendesha mashtaka wa serikali aondolewe kwenye kesi hiyo.

Zuma hakuwepo katika Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg kutokana na "dharura ya kimatibabu", wakili wake Dali Mpofu aliiambia mahakama siku ya Jumatatu.

Msemaji wake baadaye alisema kuwa Zuma alikuwa amelazwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Wawakilishi wake wa kisheria waliomba kuanza kwa kesi hiyo kuahirishwa hadi Mahakama ya Juu ya Rufaa iamue kuhusu juhudi za Zuma kutaka mwendesha mashtaka wa serikali Billy Downer aondolewe kwenye kesi hiyo.

PIA SOMA:

- Afrika Kusini: Jacob Zuma akana mashtaka ya ufisadi mwanzoni mwa kesi yake


Chanzo: Aljazeera
 
Back
Top Bottom