Rais wa Baraza la Maaskofu wakatoliki Tanzania (TEC), askofu Tarcisus Ngalalekumtwa amesema tafiti zinaogopesha wasomi wa Tanzania na Afrika, kutokana na mabara mengine kudai Afrika inachangia elimu duniani kwa asilimia mbili tu.
Alisema ni aibu kwa wasomi wa kitanzania wenye shahada za uzamili na shahada ya uzamivu (PhD), kuambiwa wamekuwa watumiaji wa elimu na si watafutaji wa elimu na kwamba hawawezi kufanya utafiti.
...
Ngalalekumtwa alikuwa akizungumza juzi kwenye mahafali ya ya tisa ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU), nje kidogo ya Manispaa ya Moshi...
MY TAKE:
Kama Africa nzima inatoa hiyo 2%, Je Tanzania inatoa kiasi gani?