Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba anawalazimisha walimu kuchangia mitihani ya utamilifu ngazi ya mkoa kwa pesa za kutoka mifukoni mwao. Afisa huyo ajulikanaye kwa jina la Samuel Mshana ambaye amehamia kwenye halmashauri hiyo hivi karibuni akitokea Halmashauri ya wilaya ya Meatu mkoani Simiyu amekuwa akiwafokea na kuwatisha walimu wakuu kwamba atawashusha vyeo wale wote watakaoshindwa kulipa mchango huo kabla ya tarehe 31 mwezi huu.
Mitihani hiyo ya utamilifu ngazi ya mkoa wa Mtwara ni kwa wanafunzi wa darasa la VII na IV ambapo inagharimu jumla ya shilingi za kitanzania 3096 kwa kila mwanafunzi. Kuna shule zinalazimika kulipa zaidi ya shilingi 900,000.
Ukiachana na malalamiko ya kuchangishwa pesa toka mifukoni mwao, pia walimu wakuu niliowasiliana nao wamebaini ubadhirifu mkubwa kwenye michango hii kwani wanafunzi wa darasa la VII na wale wa darasa la IV wanatakiwa kuchangia kiwango sawa yaani shilingi 3096 kwa kila mmoja wakati mtihani mmoja wa darasa la IV huwa na maswali yasiyozidi 25 na kwa darasa la VII mtihani mmoja hubeba maswali 50. Kwa mantiki hiyo hata idadi ya kurasa inatofautiana kati ya mtihani mmoja wa darasa la IV na ule wa darasa la VII.
Ni dhahiri ya kwamba mtihani mmoja wa darasa la VII utakuwa na idadi kubwa ya kurasa ikilinganishwa na ile ya darasa la IV. Sasa imekuwaje hata gharama za uchangiaji zifanane? Kwenye suala hili la ubadhirifu mhusika mkuu ni Afisa Elimu wa mkoa ambaye ndiye hufanya mapendekezo ya viwango vya uchangiaji na ndiye husimamia bajeti ya mkoa.
Kiujumla kuna makorokoro mengi kwenye mitihani hii inayosababisha maumivu makali kwa walimu wakuu. Hivi kwanini huyu Afisa Elimu wa wilaya asisubiri pesa za ruzuku ya uendeshaji zifike mashuleni na ndipo walimu wachangie au kumalizia madeni yao?
Waziri wa TAMISEMI Mh. Bashungwa wanusuru walimu hawa tafadhali. Hali ya maisha kwa sasa ni ngumu sana. Hawa walimu wanawezaje kulipa utitiri huu wa michango kwa pesa za mfukoni?