Afisa Elimu Igunga anawajua walimu wenye vyeti feki, Waziri Ndalichako mtumbue haraka

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,914
30,972
Wahusika wa tamisemi, Naomba kasome barua aliyoandika afisa elimu wilaya ya Igunga kuwambia walimu wajisalimishe wenye vyeti feki.

Cha ajabu ukiendelea utaona anahimiza wawahi wenyewe sababu wapo na wanajulikana

Afisa elimu unamjua mwenye vyeti feki umekaa kimya!! Wewe ni jipu tena usaa umeshaiva mama.

Ile barua imeshafika mbali na nakujuza ustuke.

Kila la kheri.
 
Mdau,waziri wa elimu hahusiki na afsa elimu.
Afsa elimu yupo chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri na waziri wa TAMISEMI
 
Niliiona ile barua,inaonyesha maafisa Elimu tulionao.Wengi wapo hivyo.Warudishwe shuleni wakafundishe,ili Wizara ifanye utaratibu wa kuwapata Maafisa Elimu wenye sifa za kuongoza wilaya
 
Haya ndio mambo mzee mengi kawashauri watendaji wa serikali kua wawe wanafanya kazi huku nafsi zao zikiwa zimetulia na sio kuwaza sifa au kuogopa kutumbuliwa.Leo yenyewe mzee kimei wa CRDB anasema kukutana na raisi ni kama kukutana na mungu.Sasa huu si upuuzi.Mungu hawezi kufananishwa na raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…