Nipe Maji
Member
- Mar 25, 2025
- 63
- 41
Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuepuka tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono sambamba na kuacha kutumia vitoweo vya wanyama kama Nyani pamoja na Ngedere ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Mpox.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa afya halmashauri ya wilaya ya Makete na msimizi wa afya kinga katika idara ya afya Boniface Sanga wakati akizungumza na Green FM Aprili 3, 2025 juu ya uwepo wa ugonjwa wa Mpox ambapo amesema kwa kuwa ugonjwa huo unatokana na wanyama hao ni vema wananchi wakaacha kula viteweo vya wanyama hao sambamba na kuacha kugusana kwani ugonjwa huo huenezwa kwa njia ya majimaji kutoka kwa mgonjwa wa Mpox kwenda kwa mtu mwingine.
Pia amesema kwa kawaida huo ni ugonjwa wa wanyama na sasa umeanza kuenezwa kutoka kwa wanyama hao kwenda kwa binadamu hivyo wananchi wanaowinda wanyama kama Ngedere,Swala wa Msituni pamoja na Nyani kuacha kula nyama yao.
Sanga ameongeza kuwa tayari halmashauri imeunda kamati maalumu ya kushughulikia changamoto hiyo endapo itakuwa kubwa na kueleza kuwa mpaka sasa tayari wananchi wameanza kuwaripoti watu wanaowahisi kuwa na dalili za ugonjwa huo na serikali imefanikiwa kuwasaidia wagonjwa hao ambapo ameweka wazi kuwa hawakuwa na ugonjwa huo baada ya kujiridhisha wakati wa matibabu hayo.
Ametaja dalili za ugonjwa huo ni mtu kuwa Upele mwili mzima,homa kali,kuwa na vidonda kwenye koo,kuhisi maumivu ya mgongo na misuli,na kuhisi kuwa na uchovu wa mwili hivyo kwa yeyote atakayebainika na dalili hizo kuripotiwa katika mamlaka za afya ili aweze kuchukuliwa na kusaidiwa.
Baadhi ya wananchi walizungumza na Green FM Daniel Sanga na Charles Lusekelo wameunga mkono kauli hiyo ya serikali na kuomba iongeze juhudi katika kudhibiti hali hiyo kwa kutoa zaidi elimu na ushauri kwa wananchi wote.