Afande Sele na O-Ten walikuwa na story moja?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,172
KWENYE "MKUU WA MKOA" O TEN anasikika akisema;
" Nakaa na mama wa kambo, sikufahamu CHOCHOTE
Kumbe si mama mzazi, sikutambua LOLOTE
ETI MAMA'NGU ALINITOSA, MOLA AKANIONGOZA..."
"TOKA NINA MWAKA MMOJA NILITOSWA NA MAMA"
Kwenye"MIMI" O TEN anasikika kwa mara nyingine akisema
"KAMA NI KUFA NINGEKUFA BADO MDOGO
MAMA'NGU ALIPONIACHA MIKONONI MWA DINGI YANGU...
WANANIAMBIA BADO YUPO"

Sasa ...
SELE ana ngoma yake iitwayo MKUKI MOYONI ambapo humo ndani anasimulia kuwa mama yake alimkimbia.
"MAMA ALISHAKIMBIA NA AKANIACHA PEKE YANGU
NATESEKA KIVYANGU MCHANA JUA NI LANGU, USIKU MVUA NI YANGU"
"TENA KUNA GAZETI LILITOA HADI PICHA ZAKE
WAUNGWANA WALIPOZIONA WALISEMA YUPO KIGOMA"

Kwa wanaojua... Ngoma hizi zilichangia ugomvi wa wawili hawa ama ni mgongano wa mawazo ambao haukuwa wa moja kwa moja kwa kuwa mwisho na mwanzo wa hadithi za wawili hawa haukuwa sawa??
Ukitazama kwa makini, wawili hawa wanautambua sana uwepo na nguvu ya mama katika malezi ya mtoto hususani katika nukuu hizo hapo JUU

Una KUMBUKUMBU gani ama ushuhuda gani kuhusu ngoma hizi?
1716885540883.jpeg
 
Mbona hizo nyimbo zimetoka nyakati tofauti , Mkuu wa mkoa ilikuja baadaye sana wakati ECT haipo tena!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom