Afande Sele FT Mr. Nice - Mimi na wewe basi

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Sep 15, 2024
137
141
images-46.jpg
images-45.jpg
AFANDE SELE FT MR. NICE
( MIMI NA WEWE BASI)

CHORUS ( MR NICE)

Ahadi yangu mimi na wewe ilikuwa ni kuishi wawili/ ( afande sele) - "Aah"
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi /... ( Afande sele) - "Basi" ×2
Nakupenda sana na bado Roho yaniuma/ eeeh
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi/ (" Afande sele ) - " Basi" ×2

VERSE..1 ( AFANDE SELE)

Mimi na wewe Basi /naposema Basi na maana mambo ni basi / sitaki tena hadithi unaso sema una ni miss/ kama unataka Sex ni basi / kwangu utakachopata kiss/ na unapotaka kiss 💋 / nitakupa 💋 kiss kwa vile nilikupenda tu/ na kwa ofisi sikupi denda / sioni wa kuniuliza eti kwanini nimekuacha/ mambo uliyoyafanya yalifanana kama picha za sinema/ mama huruma kila aliyekutaka ulitiki bila noma/ nikikutazama moyo unaniuma/ kwa zangu nyingi Gharama / we mwanamke Gani uliyekosa shukurani/ kila ulichotaka nilikupa / nikikosa naenda kopa/niku ridhishe wewe/ zaidi yangu mimi mwenyewe/ kumbe uliniona mshenzi/ sielewi mapenzi/ uka gawa penzi kama dozi/ sio siri mengi nilistamiri/ ila kwa hili ndio kwaheri/ basi hivyo mimi na wewe basi mama.../ basi hivyo mimi na wewe basi mama....!!!

CHORUS ( MR. NICE)

Ahadi yangu mimi na wewe ilikuwa ni kuishi wawili/ ( afande sele) - "Aah"
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi /... ( Afande sele) - "Basi" ×2
Nakupenda sana na bado Roho yaniuma/ eeeh
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi/ (" Afande sele ) - " Basi" ×2

VERSE..2 ( AFANDE SELE)

Mimi na wewe basi/japo naumwa na moyo/ nikikumbuka siku ambayo/ nilipokutana nawe mara ya kwanza/ mambo mengi nilikueleza/ wakati nakutongoza/ shahidi yangu mungu mkuu/ kwamba mimi sina kitu/ na ndo maana sina makuu/ napenda pesa na wewe sister Du/ ukanijibu no sweat/ uko tayari kuwa na mimi/kuwa nami kila wakati /japo ziko fit, nilijazatiti kwa vigili vya manati/niweza kukudhibiti, kwa gift 🎁 /mara sketi mara 👖 jeans .............../ huku navuta siku / na ninapozikamata maisha yetu Beer na kuku/ kumbe hauna lolote unachanganya huku na huku/ mchana kwangu na usiku kwa mwezangu / napiga magoti nasali namuomba Mungu/ niweze kukusahau , japo ni vingumu/ itanilazimu kudharau , nione kama Rafiki/ sitaki penzi la unafiki/ 💖 niache mimi mnyonge / bora nika bebe zege/ nikishindwa nianzishe genge / kuliko kupigania mapenzi nikaonekana kama bwege/ napigana kwa hela / kwa maana ndio inanipa kula & kulala /.. basi hivyo mimi na wewe basi mama

CHORUS ( MR. NICE)

Ahadi yangu mimi na wewe ilikuwa ni kuishi wawili/ ( afande sele) - "Aah"
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi /... ( Afande sele) - "Basi" ×2
Nakupenda sana na bado Roho yaniuma/ eeeh
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi/ (" Afande sele ) - " Basi" ×2

VERSE...3( AFANDE SELE)

Mimi na wewe basi / Na ninasema kwa upole/ Baby mimi nina sema sory/ nenda kwa yule/ upate kuishi nae milele/ uone atakupa nini..?/ zaidi ya nilichokupa mimi/ madem wa Uswahilini hawakosi ulimbukeni/ wana babaika sana hata kwa simu za mkononi/mi mwezenu Tena basi/ natafuta wa ushoani na ndio maana niko makini/ utadhani Soldier Vitani / niulize kwa nini dem mzuri si mtamani/ wazuri ndo wabaya, na malaya no so muhitaji/ mwanamke mubabaikaji/ nikuacha kwa hi hari , I wished you kila Raha heri/ unionapo tu popote we niulize tu afande habari /niulize sele hali ,nitakujibu tu bila Taabu/ ila kwa sasa sitaki tena unipe Adhabu / basi hivyo mimi na wewe basi mama..

CHORUS ( MR. NICE)

Ahadi yangu mimi na wewe ilikuwa ni kuishi wawili/ ( afande sele) - "Aah"
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi /... ( Afande sele) - "Basi" ×2
Nakupenda sana na bado Roho yaniuma/ eeeh
Kwakuwa umebadilika mimi na wewe Basi/ (" Afande sele ) - " Basi" ×2

Ukwaju wa kitambo

0767 542 202
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom