LGE2024 Ado Shaibu: Umoja wa CUF na ACT Wazalendo ni Hekima itokayoikomboa Nakapanya

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,452
3,761
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amepongeza hatua ya kihistoria iliyochukuliwa na viongozi wa vyama vya CUF na ACT Wazalendo katika kijiji cha Nakapanya, kata ya Nakapanya, wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, kwa kuamua kuweka tofauti zao za kiitikadi pembeni na kuungana katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza Jumapili, Novemba 24, 2024, katika mkutano wa kampeni wa CUF, Ado amesisitiza kuwa umoja huo ni mfano wa hekima ambayo viongozi wa ngazi za chini wanaweza kuwa nayo, hekima inayoweza kuwa na matokeo chanya kwa maendeleo ya Tunduru.

"Kuna nyakati viongozi na wanasiasa katika ngazi za chini wanaweza kuwa na hekima sana itakayoikomboa Tunduru kuliko hekima ambazo sisi viongozi wakubwa wa kitaifa tunazo. Ninataka wakubwa wenzangu waelewe viongozi wa ACT, CUF, viongozi wa vyama hivi waupate ujumbe kwamba Nakapanya wameamua kuweka tofauti zao pembeni na kuutafuta ukombozi wake. Hongereni sana, na hii ndiyo sababu iliyonifanya mimi kuja kwenye huu mkutano wa chama cha wananchi (CUF)."

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa hatua ya kuungana kwa vyama hivyo haipaswi kuwa ya jukwaani pekee, bali ni lazima iendelezwe kwa vitendo vya mshikamano na ushirikiano wa hali na mali.

"Niwaambieni, kuunga mkono hakutaishia jukwaani. Nitawaunga mkono kwenye umoja wenu huu kwa hali na mali."

Ado pia amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kutumia mbinu mbalimbali katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kuweka pembeni tofauti za kiitikadi ili kupambana kwa pamoja dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Back
Top Bottom