ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Ado Shaibu: Aweka Wazi Wajumbe wa Sekretarieti ya ACT-Wazalendo.
UTANGULIZI
Jana tarehe 7 Machi 2024, Halmashauri Kuu ya Chama ya Chama cha ACT Wazalendo ilikutana kwenye kikao chake maalum kilichofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo katika Jengo la Maalim Seif (Makao Makuu ya Chama) Dar es Salaam.
Kikao hiki cha Halmashauri Kuu ya Chama kimekutana baada ya Mkutano Mkuu Taifa uliofanyika kwa mafanikio makubwa utarehe 5 na 6 Machi, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Chama imefanya uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama wa kuchaguliwa kutoka kwenye Kanda 10 za Chama na teuzi mbalimbali kama ifuatavyo;-
1. UTEUZI WA KATIBU MKUU NA MANAIBU KATIBU MKUU
Kwa kuzingatia Madaraka yake chini ya Ibara ya 87(1), na 76(1)(b) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imeidhinisha uteuzi wa Ndugu Ado Shaibu Ado kuwa Katibu Mkuu wa Chama kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Kwa upande wa Manaibu Katibu Wakuu, Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imeazimia kuwa uteuzi wao ufanyike kwenye Kikao kijacho cha Halmashauri Kuu.
2. UCHAGUZI WA WAJUMBE WA KAMATI KUU
Halmashauri Kuu ya Chama imefanya uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu 24. Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo, Halmashauri Kuu ya Chama inachagua Wajumbe wawili (mmoja mwanamke na mmoja mwanaume) katika Kanda 10 za Chama upande wa Bara na wajumbe wanane (wawili wanawake na wawili wanaume) katika Kanda mbili za Zanzibar (Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba).
Hivyo basi, Kamati Kuu ya Chama iliyochaguliwa ina asilimia 50 ya Wanaume na asilimia 50 ya Wanawake.
3. UTEUZI WA WAJUMBE WA KAMATI KUU
Kwa kuzingatia madaraka yake chini ya Ibara ya 83(1)(c) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Kiongozi wa Chama amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ambao umeidhinishwa na Halmashauri Kuu. Walioteuliwa ni Ndugu Mansoor Yusuph Himid, Joran Lwehabura Bashange na Kulthum Jumanne Mchuchuli.
4. UTEUZI WA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU
Kwa kuzingatia madaraka yake chini ya Ibara ya 75(1)(l) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Othman Masoud Othman amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Taifa ambao uliidhinishwa na Kamati Kuu ya Chama. Walioteuliwa ni Ndugu Marry Zakaria na Ndugu Mgeni Jadi Kadika
5. UTEUZI WA SEKRETARIETI YA CHAMA
Halmashauri Kuu ya Chama Taifa kwa kuzingatia madaraka yake chini ya Ibara ya 76(1)(c) na Ibara ya 89A ya Katiba ya ACT Wazalendo imefanya uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Chama, Makatibu wa Idara na Manaibu Katibu wa Idara za Chama kama ifuatavyo;-
(i) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Chama:
• Wakili Bonifasia Aidan Mapunda
(ii) Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma:
• Katibu: Salim Abdalla Bimani
• Naibu Katibu: Shangwe Mika Ayo
(iii) Idara ya Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi
• Katibu: Omary Ali Shehe
• Naibu Katibu: Esther Akoth Thomas
(iv) Idara ya Fedha
• Katibu: Rachel Lawrence Kimambo
• Naibu Katibu: Hafidh Bakar Abdulrahman
(v) Idara ya Mambo ya Nje
• Katibu: Mwanaisha Zuberi Mndeme
• Naibu Katibu: Nasra Omar Nassor
(vi) Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi
• Katibu: Shaweji Mketo
• Naibu Katibu: Pavu Juma Abdallah
Makatibu wa Ngome za Chama
(i) Katibu Ngome ya Vijana: Mohamed Busara
(ii) Katibu Ngome ya Wazee: Janeth Fusi
(iii) Katibu Ngome ya Wanawake: Fatma Ferej
Idadi ya wanawake katika Sekretarieti ni 60%
6. UTEUZI WA MKAGUZI MKUU WA NDANI
Halmashauri Kuu ya Chama kwa kuzingatia madaraka yake chini ya Ibara ya 76(1)(o) imemteua Ndugu Abdallah Bakar Hassan kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani (Internal Auditor).
7. MWENENDO WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR
Tathmini ya kina iliyofanywa na Halmashauri Kuu ya Chama inaonesha kuwa, ukiacha suala la kuachiwa huru kwa wanachama waliokuwa wanashikiliwa kutokana na uchaguzi mkuu 2020, hakuna hoja hata moja ya mageuzi ya kimfumo kati ya hoja tatu zilizowasilishwa ambayo imefanyiwa kazi na Rais wa Zanzibar Ndugu Hussein Mwinyi. Hoja zilizowasilishwa ni fidia kwa wahanga wa uchaguzi mkuu 2020, kuundwa Tume ya Kijaji kuchunguza uvunjifu wa haki za binadamu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na mageuzi katika mfumo wa uchaguzi.
Halmshauri Kuu ya Chama Taifa kwenye kikao chake cha tarehe 4 Machi, 2024 ilitoa agizo kwa Kamati ya Uongozi Taifa kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kuwaeleza juu ya uamuzi wa Chama cha ACT Wazalendo kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na kutotekelezwa kwa makubaliano yaliyoingiwa na Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa niaba ya ACT Wazalendo na Rais Mwinyi kabla ya ACT Wazalendo kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Imetolewa na:
Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo,
08 Machi 2024.
Dar es Salaam.