Adhabu mbaya kabisa kupata kutokea kwa mtu ambaye alitembea na mke watu mtu. Na aliyetembea na mume wa mtu

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,306
Nlikuwa weekend nimeka mitaa flan nakunywa na jamaa zangu kistaarabu tu. pembeni yetu walikuwepo wanadada watatu ambao walikuwa wakipiga story kuhusiana na mambo ya fumanizi mbalimbali. nasi tukajikuta tunaongelea jambo hilo. jamaa yangu mmoja akasema yeye ni bora umfanye jambo lingine lolote ila si kutembea na mkewe.kwamba kwa hilo hawezi kukusamehe.

katika maongezi nikakumbuka kisa kimoja nlikisoma miaka ya 1990s hivi huko mexico.bwana mmoja ambaye alikuwa ni mtu mwenye uwezo mdogo akifahamika kwa jina la julio alifanikiwa kuoa mke mzuri sana walipendana. julio alikuwa ni dr baadaye akapata msala na kusimamishwa kazi...yakaanza maisha ya shida n kumfanya mkewe kuingia kwenye ushawishi na kuanza kutoka na jamaa mwingine mwenye uwezo kiasi flan wa kipesa. julio alienda kwa mhusika kwanza na kumwambia yeye anafahama udhaifu wa wanawake so kaamua aongee na mwanaume mwenzie kuwa amwachie mkewe maana yeye yule bwana ana weza pata mwanamke mwingine yeyote ila yeye ndo kampata huyu na anampenda. jamaa alicheka tu kwa dharau na kwa lugha ya leo angemwambia "pambana na hali yako" akamnanga sana na kumwambia akamwambie hayo maneno mkewe yeye anakula mzigo kama kawa.

julio aliondoka kwa unyonge sana akarudi nyumbani kwake. jambo moja la ajabu hakumwambia mkewe. akawa anaendelea tu na issues zake.yule tajiri naye hakutaka kumwambia mke wa jamaa ili nadhani asimpe waswas alipoona mke wa jamaa hajamwuliza anything naye hakumwambia kuwa mumewe alimfuata.

siku ya siku jamaa tajiri alikuwa anaendesha gari yake jioni anarudi kwake..kulikuwa na ka giza flan hivi akakuta njiani kama kuna mti uliangukia barabarani umeziba njia. basi akaamua kushuka kwenda kusogeza. julio alikuwa tayari amejipanga alitokea kichakani na kumpiga na kitu kigumu kichwani. tajiri alianguka. julio alimbeba begani akaingia naye kichakani ambako alikuwa amepaki gari lake akaondoka naye kuelekea kwenye nyumba yake moja iliyoko shambani umbali kama wa km 30 hivi.

julio alikuwa ni daktari ambaye aliachishwa udaktari kutokana na kuwa alihusika kwenye tukio la kushawishi wenzie wagome.so baada ya hapo hakuweza pata kazi tena...na akaamua kujihusisha na kilimo tu. hivyo huko shambani alikuwa amejenga nyumba ndogo hivi ya kupumzikia siku wanapoenda shambani kifamilia. akaenda na yule mgoni wake na kumweka kwenye store huku akiwa amemfunga mikono na miguu kwa pingu na kamba pia. akamweka kule ndani na siku ile ya kwanza alimkata viganja viwili vya mikono.kisha akamweka dawa na kumfunga vizuri damu isitoke

siku hiyo alirudi kwake usiku akiwa amechoka. usiku ukapita. kesho yake tena alienda kule shambani asubuh alimkuta mgonjwa akiwa hoi hasa. akampatia na chakula na dawa. inasemekana siku hiyo alimkata miguu yote miwili hii sehemu ya kuvalia viatu, akamkata ulimi,akamtoboa macho,akamkata na masikio yote,kisha akamkata uume. na humo mote alikuwa akipaka dawa ya kuzuia damu isitoke na kisha akafunga. alipomaliza akaondoka kurudi nyumbani. muda wote alipokuwa anafanya shughuli hizo alikuwa anavua nguo zote anabaki uchi kabisa. akimaliza anaenda anaoga anavaa nguo zake anarudi kwake.

siku hiyo usiku aliporudi nyumbani mapema kidogo katika shampoo ya mkewe alienda akamimina dawa flan mbayo mkewe alipoenda kuoga kwa kutumia ile shampoo ilimpofusha macho na kumuunguza usoni kwa kiasi kikubwa sana. usiku huo huo jamaa aliondoka pale home na kwenda kusikojulikana. akiwa njiani alipiga simu kuwataarifu polisi kuwa waende kutembelea nyumba namba flan na pia akawaelekeza kule shambani kwake.waende na ambulance. jamaa walipoenda walimkuta mhusika akiwa amezimia akiwa amekatwa viganja,sehemu ya chini ya miguu,masikio,ametobolewa macho,amekatwa ulimi na uume pia. julio hakupatikana ameenda wapi.

baada ya miaka kumi 5 julio aliandika ujumbe mrefu sana na kuutuma kwenye gazeti moja nchini mexico akielezea kisa chote na kusema ameshamwomba Mungu msamaha na wale aliowaadhibu kwa adhabu kali kiasi kile. yule mgoni tajiri inasemekana alihudumiwa vizuri hosp akapona. ila alikuja kujiua kwa kujidumbukiza kwenye swimming pool lile lile alilokuwa aki enjoy na mke wa mwenzie.

mwanamke aliendelea kuishi kwa mateso makubwa sana maana hakuwa tena na mvuto na wanaume wengi walimchukia na kumwona ni sawa na shetani kwa vile alivyomtendea mumewe na kumsababisha julio ambaye inasemekena alikuwa ni mtu mpole sana na asiye na maneno mengi ila mwenye msimamo kutenda unyama ule. ile inasemekana ni moja ya adhabu mbaya sana kupata kutokea.

adhabu zetu za kiafrika nilizisikia kutoka kwa wale wadada ambao mmoja wapo alikuwa anamshauri yule ambaye mumewe anaibwa kuwa wala asiwaze sana. ampeleke tanga kuna mganga ambaye aliwahi kumfanya mwizi wa rafiki yake atokwe na damu na kunuka sehemu yake ya siri kwa mwaka mzima. anasema yule dada alikuwa anatembea amevaa diaper. na alikuwa ananuka kiasi kwamba alikuwa hakai na watu karibu. ile adhabu ilimfanya mwaka mzima awe mtu ambaye anajifungia ndani na akitoka ni kwenda kuhangaika na madaktari na hatimaye waganga.haikufua dafu mwishowe yule dad alikufa baada ya sehemu yake ya siri kuoza na kuanza kutoa funza. hiyo ilikuwa adhabu ya huku kwetu afrika.

nikawaza adhabu gani unaweza mpa mtu anayetembea na mkeo au mumeo akijua kabisa ila anafanya makusudi kwa kujua wewe ni dhaifu au huna cha kumfanya?

"Mwenye meno akicheka mwenye mapengo huudhika sana"


TAHADHARI: USIJE KUTEMBEA NA MKE AU MUME WA MTU UNAWEZA KOJOA DAGAA.
 
mm nasemaga tu nisimfumanie mke wangu maana akili zangu nazijua mwenyewe tu
 
Kunamdau Mjaa humu alitoa Angalizo lifuatalo
"Kamwe Usije ukachefuliwa na maamuzi aliyefanya mwenza wako..tena akiwa na akili timamu/bila uwoga wowote..kuamua kuliwa au kula tena kwa kuburudika sawia"
Kwanini..Sababu nawewe utaingia katika mtego mwingine wa dhambi ambayo itakupotezea maisha au muelekeo wako wa kimaisha..sababu ya maamuzi yakipumbavu yaliotokana na wapumbavu wawilii..

Mimi kama Mwanaume endapo ntafahamu mke/mwenza wangu ameliwa au analiwa..Lakufanya ni moja tuu...Ntadeal na mwenza wangu tuu..Yeye ndie atakaenipa hadidu rejea kabla ya maamuzi yangu..
 
Maelezo mengii ila tu nakuinga mkono kuwa ni dhambi.amri imesema usitamani ng'ombe wa jiran yako wala mnyama,wala mjakazi,wala mke wake wala chochote kilichopo malangon pake.
 
Daaahhh lakini hii kitu km huwezi kuvumilia bora ufanye umafia km julio alivyofanya!ndo utaishi kwa amani maisha yako yaliyobaki
 
Kama stories za akina shigongo vile!!! Lakini inafundisha pia,,asante kwa kutujuza mambo ya julio
 
Nilishuhudia kitaa mgoni alif***a live na kiuno akainamisha, ila majanga yalimkuta mfir**ji baada ya mwaka akapewa ukimwi wa kichawi jamaa tumemzika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom