Adeline Lyakurwa: Ndege alinasa kwenye nyaya za umeme, mafundi wamerekebisha, umeme umerejea Bariadi (Simiyu)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580
4ac95038-0d0f-4557-af14-b8e3e52f2669.jpg

Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa anatokea Wilaya ya Bariadi, Kijiji cha Mwasinasi kulalamika kuwa kuna kero ya kukatwa Umeme bila taarifa na shida hiyo imekuwa ikijirudia tangu wakati kuna Mgawo wa Umeme, ufafanuzi umetolewa na imeelezwa changamoto hiyo imetatuliwa.

Afisa Uhusiano wa TANESCO, Mkoa wa Simiyu, Adeline Lyakurwa amesema “Timu ya mafundi ilienda eneo la tukio jana (Septemba 2, 2024) na jioni yake umeme ukarejea.

“Changamoto iliyokuwepo kwenye ‘line’ baada ya mafundi kwenda ‘kupatrol line’ maeneo yaliyoelezwa kuwa na changamoto pamoja na kusababisha maeneo tofauti yaliyolalamikiwa kukosa umeme pamoja ya aliyeleta kero ya kukatikakatika kwa umeme, sasa Wana umeme.

Pia soma:
~ TANESCO- Simiyu yatuma Wataalam kufuatilia changamoto ya umeme Kata ya Muamatondo - Bariadi
~ Kata ya Muamatondo wilaya ya Bariadi suala la umeme kukatika limekuwa kero sana
5c2bbf09-95b5-45bd-a8b7-b937b5d27224.jpg

“Kulikuwa na ndege pia aliyenasa kwenye umeme, kulikuwa na waya wa earth huku pia insulators zikitoa kwenye sehemu yake inapotakiwa, zikakutwa zimening'inia kwenye waya.

“Baada ya kumwondoa ndege na kurekebisha miundombinu, huduma ilirejea na ni maeneo tofauti,

tunawasisitiza wakipata hitilafu yoyote watoe taarifa kupitia namba zetu za mkoa na makao makuu.

"Niwaombe Wananchi wanapokuwa na changamoto wanaweza kupiga simu kwenye namba 0734013113, 0748550000 ambayo pia inapatikana kwa njia ya WhatsApp, kwa maombi ya umeme pakua NIKONEKT App au piga *152*00#.”

87d0413a-c53c-4800-9da1-b9fc83145c1e.jpg

bb7a0491-594d-4f8b-90eb-63b7f1bb7b37.jpg
 
Back
Top Bottom