LGE2024 ACT Wazalendo yadai viongozi wake kutekwa na kukamatwa, haya yataisha lini?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
296
545
Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali matukio kiliyoyaita ya kutekwa, kukamatwa, na kutishiwa kwa viongozi wake katika maeneo mbalimbali nchini, huku kikitaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha usalama wao.

Rahma Mwita, Msemaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa ACT Wazalendo ameeleza katika taarifa iliyotolewa Novemba 26, 2024 kuwa tukio la hivi karibuni lililotokea tarehe 25 Novemba 2024 huko Geita, limewahusisha Paulo Matayo na Staifodi Mwesigwa, Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee wa chama hicho, ambao wanadaiwa kutekwa usiku na baadaye kupatikana wakiwa mikononi mwa polisi.

“Matukio haya ya utekaji na kukamatwa kwa viongozi wetu ni kinyume na misingi ya haki, usawa, na sheria za nchi. Vyombo vya dola havipaswi kuwa silaha ya kuzima sauti za kisiasa au kudhoofisha juhudi za demokrasia”, ameeleza.

Kwa mujibu wa chama hicho, tukio hilo limefuatia tetesi za kuwepo kwa mpango wa kuwapoteza vinara wa chama hicho katika Jimbo la Muleba Kusini. Aidha, tukio jingine lililoripotiwa ni kukamatwa kwa Mohammed Kapopo, mgombea wa uenyekiti wa Kitongoji cha Maholela, Jimbo la Tunduru Kaskazini, kwa tuhuma za uchochezi.

Soma pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Njombe aeleza A-Z mkasa nzima ilivyotokea mpaka Freeman Mbowe kukamatwa na Polisi

Rahma ameendelea kusisitiza kuwa vitendo hivyo vinaashiria mpango wa kuwazuia viongozi wa ACT Wazalendo kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuwaachilia viongozi wa ACT Wazalendo mara moja na kuhakikisha wanarejea kwenye shughuli zao za kampeni na Uchaguzi. Demokrasia imara inajengwa kwa usawa na haki kwa wote,” ameongeza.

Chama hicho pia kimezitaka mamlaka kuwajibika katika kuhakikisha usalama wa viongozi na wanachama wake.
Screenshot 2024-11-26 155319.png

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom