Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,586
TAARIFA KWA UMMA
Tumeendelea kupokea matukio hujuma kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Utekaji, ukamataji kinyume cha sheria, kura feki, na kusumbuliwa kwa mawakala.
===
KURA FEKI
Kumekuwa na ukamataji wa kura feki nyingi maeneo mbalimbali nchini ambazo tayari zimepigwa na kukichagua Chama cha Mapinduzi kama kiongozi wa eneo husika. Maeneo yaliyokamatwa kura feki ni Mwandiga, Mbarali, Kahama Mjini, Kigoma Mjini, Arusha Mjini, Geita na maeneo mengi nchini.
MAWAKALA KUTOLEWA NJE NA KUHITAJIKA UTAMBULISHO WA MTENDAJI WA MTAA.
Maeneo mbali mbali nchini mawakala wetu wametolewa kwenye vituo kwa kudaiwa hawana barua za utambulisho au wakatafute utambuilisho wa mtaa maana sio wakazi wa eneo husika. Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na kadhia hii ni Arumeru Mashariki, Mitaa yote ya jimbo la Moshi Mjini, Tunduma na maeneo mengi nchini kinyume na utaratibu.
UKAMATAJI HOLELA
Kumekuwa na ukamataji holela wa wanachama, wagombea na viongozi wa ACT-Wazalendo kwenye maeneo mbalimbali ya uchaguzi; baadhi ya maeneo hayo ni Temeke, Mbagala, Kinondoni, Arusha Mjini, Katavi, Pangani, Kigoma Mjini, Muleba Kusini, Mchinga, Tunduru na maeneo mengine nchini wamekamatwa na jeshi la polisi bila sababu ya msingi.
WAGOMBEA KUTOKUONEKANA KWENYE KARATASI YA KUPIGIA KURA
Kuna baadhi ya maeneo wagombea wa ACT-Wazalendo hawakuepo kwenye karatasi ya kupigia kura, baadhi ya maeneo hayo ni Kilwa, Nanyamba, Muheza, Uvinza na maeneo mengine hili lilipelekea zoezi la uchaguzi kusimama kwa muda.
KUWEPO KWA MADAFTARI HEWA NA UTUMIAJI WA VITAMBULISHO PAMOJA NA MADAFTARI YA KATA TOFAUTI KUPIGA KURA
Kuna maeneo mawakala wetu wamekamata madaftari hewa, madaftari ya kata ingine kuletwa kwenye kata tofauti ili majina yatumike kuwapigia kura wagombea wa CCM, watu wasio kuwa na kituo husika kuja kupiga kura kituo kingine kuongeza idadi ya wapiga kura pamoja na wasimamizi wa uchaguzi kudai vitambulisho na kuwaruhusu watu kupiga kura bila jina na wamekuja na vitambulisho tofauti na utaratibu. Mtaa wa Idrisa, Mtaa wa Mtambani, Mtaa wa Mwinyimkuu na Kijiji cha Sale ni baadhi ya maeneo yaliyogundua mbinu hizi.
KUWEPO KWA VITUO HEWA
Kumekuwa na uwepo wa vituo hewa tofauti na vituo vilivyotangazwa awali, Mtaa wa Mpakani Kata ya Mbagala Kuu Temeke walitangaza vituo vya kupigia kura 10 lakini vituo vinavyoonekana 7 na vituo 3 havikujulikana vipo wapi mpaka baada ya mvutano wa muda wakaambiwa vituo vipo Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu majira ya saa 4 asubuhi na kukuta maboksi ya kura yamejaa.
KUTEKWA KUPIGWA NA KUVAMIWA KWA MAWAKALA NA VIONGOZI
Kuna maeneo viongozi wa ACT-Wazalendo wametekwa na kupelekwa kkusikojulikana. Mfano Jimbo la Mchinga mwenyekiti wa ngome ya wanawake wa jimbo ametekwa na gari aina ya landcruiser T133GEE akiwa kwenye harakati za kufuatilia mwenendo wa uchaguzi na kupelekwa kusikojulikana. Lakini pia Katibu wa Mkoa wa Arusha amepigwa na vijana wa CCM akiwa kituoni kama wakala na kumtoa eneo analosimamia uchaguzi, Katibu wa jimbo la Igunga na wengine wengi wamepigwa na kuvamiwa na vijana wa CCM bila polisi kufanya lolote.
ACT Wazalendo itaendelea kuuhabarisha umma kila kinacho endelea kwenye maeneo ya uchaguzi, Chama kina laani vikali vitendo hivi kwani ni uvunjifu wa Demokrasia nchini na namna ya kupoka madaraka ya wananchi kuchagua viongozi wanao wataka.
Imetolewa na;
Rahma Mwita,
Msemaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, АСТ
Wazalendo.
27 Novemba 2024
PIA SOMA
- LGE2024 - ACT Wazalendo: Wagombea wetu 51,423 wameenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kwa sasa zoezi la upigaji kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji limehitimishwa rasmi na tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu hatua zinazofuata katika mchakato wa uchaguzi. Tumeendelea kupokea taarifa za matukio mengi ya uvunjifu wa demokrasia kwenye uchaguzi huu. Sambamba na taarifa yetu ya kwanza tuliyoitoa mapema leo mchana bado tumepokea taarifa za changamoto na kasorozilizojitokeza katika vituo kama ifuatavyo;KURA FEKI