Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,585
Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea kuimarisha kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mtakuja, Kata ya Vingunguti, Jimbo la Segerea, Dar es Salaam.
Mkutano huo, uliovutia idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo, uliongozwa na Naibu Katibu wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa na Mlezi wa Jimbo la Segerea Ruqayya Nassir ambaye alimnadi Jumanne Kilavula, mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakuja
Ruqayya amewataka wakazi wa Mtakuja kufanya maamuzi ya busara katika uchaguzi ujao wa Novemba 27, 2024, kwa kuchagua wagombea waadilifu na wenye dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo. Amesisitiza kuwa ACT Wazalendo ni chama kinachoendeshwa kwa uwazi, usawa, na kujali maslahi ya wananchi wa kawaida.
Ameongeza kuwa chama hicho kimejikita pia katika kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha nafasi za wanawake na vijana zinasimamiwa kwa haki.