Wiston Mogha
Senior Member
- Feb 13, 2014
- 168
- 141
Tunataka chunguzi kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Edgar Mwakabela
ACT Wazalendo tunalaani na kukemea vikali tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa kijana Edgar Mwakabela, mtandaoni (X) anajulikana Sativa. Mwakabela amepatikana leo tarehe 27 Juni, 2024 huko Mkoani Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya.
Kijana huyu ni mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam alitafutwa na ndugu zake bila mafanikio baada ya kutoonekana kwa siku 3 tangu Jumapili tarehe 23.
Watanzania wameanza kuingia tena na hofu kukithiri kwa matukio ya wananchi kupotea, kuteswa na kuawa kwa kasi siku za hivi karibu. Inasikitisha pia kuona Jeshi la Polisi kutochukua hatua za haraka kwa wanaohusika na matukio hayo.
Tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio hayo bila hatua madhubuti kuchukuliwa. Wananchi wamechoshwa na kutowajibika kwa Jeshi la Polisi au kuhusishwa kwao katika matukio ya kuwaumiza, kuwatesa na kuwakandamiza kila uchao badala ya kutekeleza wajibu wa kuwalinda pamoja na mali zao.
ACT Wazando tumechukua hatua za kumrejesha Dar es Salaam kwa Ndege kijana Mwakabela ili aweze kupatiwa matibabu haraka na ya kibingwa.
Hata hivyo, tunataka hatua za haraka za uchuhguzi zifanyike ili kubaini watu waliohusika na utekaji wa Ndg. Edgar Mwakabela.
Ndg. Dahlia Majid,
Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani
27 Juni, 2024.