The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 700
- 1,169
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonyesha dalili zote kuwa hakipo tayari kwa mabadiliko ya kimfumo ya uchaguzi hivyo kwa sasa wanahitaji kudai mabadiliko kwa njia ya mapambano.
Akizungumza Februari 23 kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho Semu amesema “CCM na Dola wameonesha kuwa hawako tayari kufanya mageuzi ya kuimarisha demokrasia na mifumo ya Uchaguzi yatakayopelekea kuheshimiwa maamuzi ya wananchi. Ni lazima sasa tuyadai kwa njia ya mapambano.”
Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hata hivyo ametahadarisha wanachama wa chama hicho kuwa yanahitajika maandalizi makubwa ili kuyaendea mapambano hayo pamoja na kudhibiti hujuma ambazo wamedai CCM kuwafanyia kwenye chaguzi mbali mbali
“Chama chetu kinapaswa kujipanga vizuri kuhakikisha kuwa tunadhibiti hujuma za CCM na dola na tunafanikisha malengo yetu ya kisiasa kama ambavyo majemedari hodari kwenye vita mbalimbali ulimwenguni waliweza kuusoma mwelekeo wa vita, kufufua ari ya mapambano na kusonga mbele hadi kuupata ushindi.” amesema Semu
"Kwa mshikamano wetu, kwa hakika, tutayafikia malengo yetu. Ndugu zangu, ni wakati wa kuchukua hatua. Tuwe na mshikamano na umoja katika kukabiliana na matatizo yanayotukabili. Kwa pamoja, tunaweza kufanikisha malengo yetu na kuleta mabadiliko tunayoyahitaji." amesisitiza Semu