Acha uvivu unaweza kuacha mchepuko wako kirahisi

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Wanaume ambao wanatafuta sababu za kuacha mchepuko lakini wanakosa kisingizio, tafadhali tumia moja au zaidi ya njia hizi. Ukiwa umekunja uso, muangalie mchepuko machoni kisha kwa hasira sema hivi;

1. Yaani we huniheshimu kabisa. Mi naongea wewe unaendelea kupumua. Hiyo ni dharau kubwa sana,basi bwana nenda kwa unaemheshimu.

2. Dah kwa hiyo siku hizi unakunywa koka yenye majina ya wanaume wengine, tafadhali nenda salama kamfuate mtu wako.

3. Hee umeweka wimbo wa Diamond kwenye simu,lazima kuna kitu kati ya wewe na Diamond sikutaki tena.

4. Unajua nakushangaa, nimekupigia tu na simu ilipolia mara moja tu ukapokea, inamaana huna kazi ni mtu unashinda na simu tu. Mimi watu wavivu siwawezi kwaheri.

5. Kila siku nakwambia napenda chakula kuwa cha moto wewe unaenda kuninunulia icecream ya baridi, hiyo ni dharau sikutaki tena.

6. Nimegundua huwa hutoi sadaka kanisani, sasa kama Mungu mwenyewe unamdhulumu mimi si ndio utaniua kabisa. Sikutaki tena.

7. Unajua we mwanamke wa ajabu sana, mara zote nikikukaribia unacheka unamcheka nani? Nenda kwa hao wasiochekesha.

NB: Yaani hapo msipoachana apigwe tu maana hakuna namna nyingine sasa eeeh!
 
Sijui kama watakuelewa

Na hata wakielewa sijui kama watachukua

Na hata wakichukua sijui kama watafanyia kazi ama wataweka kama pamboz
 
Dawa ya demu usomtaka ni kumuomba #TIGO tu kama wao wanavyotufanyia makusudi wakiwa hawatutaki kutuomba mihela bila sababu ili kutukomoa.
Ila sasa unakuta Janamke lingine unaliomba TIGO linakukubalia lazma uchoke.
Jingine linakwambia linapendaga ila lilikua linaogopa kukuambua.Tobaaaaaaa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom