Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,275
Leo tunakuzwa katika misingi ya kujitetea na kukwepa kuwajibika karibu katika kila eneo. Hatujifunzi na hatutaki kukubali kuwa tunapaswa kuwajibika asilimia mia moja juu ya maisha yetu na badala yake tunawatafuta wa kuwatupia lawama.
Ni kweli yapo mambo mengi yanayoweza kutokea nje ya uwezo etu ila hayaondoi wajibu wetu juu ya maisha yetu. Hatuwezi kuizuia mvua kunyesha ila tunaweza kukwepa au kujilinda mvua isituloweshe.
Mchezo wa lawama " blame game" ni mchezo wa wasiopenda kuwajibika juu yao. Ni mchezo wa kujiliwaza na kuhamishia majukumu yako kwa wengine kana kwamba na wao hawana majukumu yao. Unayemlaumu na yeye analaumu.
Umasikini na uzembe mkubwa umejificha kwenye mchezo wa lawama. Mduara mzima wa umasikini na uzembe kivuli chake kikuu na faraja yake ni lawama. Lawama hutuaminisha kuwa yupo aliyepaswa kuwajibika juu yetu na siyo sisi "anayetusaidia kuishi maisha yetu"...ah!..ah...
Lawama humfanya mtu kujiona yupo sahihi sana "malaika"'ila wengine ndiyo wanaomkosea na kumfanya kuwa alivyo. Ukweli unaouma ni kuwa "tupo tulivyo kwa sababu tunataka haswa kuwa hivi tulivyo". Hakuna lugha rahisi zaidi ya kuumiza Ili kumfanya mtu kuona uchungu juu ya hali yake na kuchukua hatua.
"You are the master of your life"