KJ07
JF-Expert Member
- Dec 17, 2021
- 2,283
- 5,195
Salaam wakuu.
Heri ya pasaka kwa wale washerehekeao na ramadhan kareem kwa wale wafungao na heri ya sikukuu ya wajinga kwa tuisubiriyo.
Niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu.
Siku kadhaa zilizopita nilikuwa natoka tegeta naelekea kariakoo kwa daladala za T/NYUKI-GEREZANI.
siti niliyokuwa nimekaa nilikuwa na mdada fulani hivi kibonge aliyekuwa na bahasha ya chips.
Gari limetembea tembea akatoa chips yake kwenye bahasha na kuanza kuifakamia chips.
Nasema kuifakamia sababu alikuwa anakula kama vile anakimbizwa.
Wandugu kama unajijua haujui kula kistaarabu basi hakikisha umekula kwenye umma wa watu wachache tena walio busy na mambo yao kama kwenye vibanda vya chips.
Na sio kwenye umma wa watu wengi maana unaweza kujikuta unatia aibu na kuwatukanisha wazazi wako kwamba hawajakufundisha kula kistaarabu.
Kibonge wa watu kamaliza kula chips zake akafinyanga finyanga ile foil na bahasha na kuitupa dirishani huku gari likiwa linatembea.
Wakati huo daladala ina dustbin na tulikuwa tumekaa mbele kabisa jirani na makazi ya konda.
Akaona haitoshi akatoa dumu la maji kwenye mkoba na akanywa na akarudia kitendo kilekile cha kutupa nje ya gari huku likiwa lianatembea.
Shame upon her. Shame upon her. Shame upon her.
Na kama unaisoma hii jua kwamba nilikumaindi.
Huyo ni mfano mmoja nilioukumbuka saa kwa harakaharaka nilipokuwa nataka kuwasilisha kero yangu.
Ila watu wa aina hii wako wengi sana tena kwenye jiji letu la Dar es salaam.
Wadada mjiheshimu aisee, mnajipunguzia point kwa vijimambo vidogovidogo vya ajabu mnavyovifanya.
Mnatia aibu.
Huwa naitafakari sana akili ya mtu ambaye anatupa taka hovyo, hii haijalishi ni kwenye daladala au penginepo.
Jambo hili limekuwa ni kama tabia sasa, mtu anakunywa energy yake anamaliza anatupa kopo barabarani.Hata kama kuna watu wa usafi, mambo mengine ni ya kuyarekebisha wenyewe hata kabla hayajarekebishwa na watu baki.
Aisee watu mnaotupa makopo ya kwenye daladala muache.
Mnatukwaza.
Mnatukwaza sana.
Inawashushia heshima sana ni hamjui tu.
Watu hawawaambii papo kwa papo kuepusha mambo mengine ila mnawakera sana.
Natamani mamlaka ziweke sheria kali zitakazowawajibisha vikali watu wanaotupa taka kwenye usafiri wa umma.
TUBADILIKE.