Abdul Nondo wa ACT Wazalendo atoa tamko kuhusu kutekwa kwake Stendi ya Magufuli

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,674
4,495
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo, anatoa tamko muda huu kuhusu kutekwa kwake Stendi ya Magufuli.

Fuatilia hapa akitoa tamko lake


View: https://www.youtube.com/live/LyTw1PpXT4I?si=Ze8FhWkwx-7UfKkb

"Baada ya kutekwa katika stendi ya Magufuli mashuhuda waliotoa taarifa ndio ambao walisaidia kwa sababu mashuhuda waliokuwa pale waliangalia vitu wakakuta ni vitu vya ACT, hawana namba za viongozi wa ACT Wazalendo lakini mashuhuda kadhaa wana namba za aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika. Na kwa sababu tukio lile lilitokea katika Jimbo la Kibamba, yeye akachukua taarifa hii kwa uzito, napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mnyika."

"Nichukue fursa hii kuwashukuru boda boda wote Tanzania wakiwakishwa na Bodaboda mwenzao aliyenisaidia pale Coco beach kwa sababu nilomba msaada kwa magari yaliyokuwa yanapita pale nikiyasimamisha nikiwa katikati ya barabara lakini hakuna magari yaliyosimama kwa sababu shati langu lilikuwa limechanika chanika suruali naishikilia labda hawakua na uaminifu na mimi, bodaboda mmoja nilipomsimamisha kumuomba msaada alienda kuchukua bodaboda wenzake na akaja kunisikiliza na wakaridhia kunisaidia"

"Nilipelekwa Aga Khan nikiwa hoi sana nawashukuru kwa huduma yao kwa kutoa huduma yao ya matibabu haraka na ya uhakika kuhakikisha figo yangu ambayo inakwenda kufeli inaimarika na kufanya kazi kwa sababu nilipofika pale waligundua kama figo inakwenda kufeli."

"Baada ya kutekwa na kuteswa na baadaye kutelekezwa Coco Beach wilaya ya Kinondoni, Abdul Nondo alipewa masharti kadhaa ambayo aliambiwa kama hatayatimiza basi atauawa. Walioniteka awalikuwa wakiniambia mimi nina mdomo, na waliponiacha Coco Beach walinipa masharti ya kwamba;"

1. Tukikuacha usieleze chochote kuhusu kutekwa kwako, nikitoka pale niende nikae kimya.

2. Nisiongee na vyombo vya habari.

3. Nisiendelee na mdomo wangu wa kuongea ongea na kuandika andika mtandaoni.

4. Nikitoka pale wanaponiacha, basi moja kwa moja niende nyumbani kabisa nikapumzike ili nikiamka asubuhi taarifa zivume kuwa Nondo kapatikana akiwa kwake amelala ili vyombo vya mamlaka vipate kusema tukio hili limetengenezwa ni uongo kwamba mtu unawezaje kutekwa halafu ukaenda nyumbani kulala.

"Masharti yote hayo waliyonipa nimeyavunja, sijatii hata sharti moja."

"Naomba niwaambie watanzania suala la ulinzi na usalama ni jambo ambalo tunapaswa tuungane kwa pamoja kupaza sauti zetu kupinga kukemea haya matendo. Na wala tusiseme kwamba haya matukio yanatokea kwa wakosoaji, viongozi wa vyama, wanaharakati kwamba wewe ambaye si mwanaharakati kwamba upo salama."

"Kwamba wewe uko ndani ya chama cha mapinduzi unajiona uko salama tunajidanganya sana namna matukio haya yalipofikia sasa hivi sio ya vyama tena yameshavuka mpaka. Tarimo (mfanyabiashara Deogratius Tarimo) hajihusishi kabisa na siasa katekwa, umeona Dunstan Mutajura hajihusishi kabisa na masuala ya kisiasa katekwa kwa hiyo tunapoendelea kukaa kimya tunazidi kuyalea haya matukio yaendelee kutokea."

"Kumekuwa na mwanya wa dhihaka na propaganda kwamba matukio haya ya utekaji sio ya ukweli ni ya kutengeneza ntu anawezaje kutengeneza kujiumiza, mtu anawezaje kutengeneza kujiumiza mguu manusura kufa"

"Nilimsikiliza hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa akisema asilimia 80% ya matukio ya utekaji ni ya kutengeneza kwamba asilimia 20% ndiyo ya kweli lakini nimezungumza hapa matukio 8 ambayo hayana uchunguzi basi kama ni ya kutengeneza fanyeni chunguzi mtuambie aliyemteka Soka, aliyemteka Sativa, aliyemteka na kumuua Ally Kibao, aliyeniteka mimi tupeni majibu"
 
Mpeni pole Sana Ila mwambie rafiki yake na mwanaharakati mwenziye bwana Emijidius Cornell Sasa Yuko Mbeya na Sasa amekuwa Kama kichaa moja haikai Wala mbili haikai amkumbuke aje amchukue Kama alivyomsaidia kumtoa Muhimbili kipindi kile aliposingiziwa ukichaa na chuo kishiriki Cha Dar es salaam (DUCE)
 
Naskia museven mbowe, anasambaza pesa huko balaa
Umemuonea sana Erythrocyte inabidi umtake radhi. Tangu mtifuano wa ngazi za kitaifa umeanza sijawahi kumsoma popote akichukua upande wowote ule, yeye amesimama na CHADEMA.
Na kama Erythrocyte angekuwa ni kibaraka wa Mbowe kama mnavyomyuhumu, basi ule uchaguzi wa Kanda mngemuona mapema sana akiwa upande wa Sugu, lakini yeye alikuwa kinyume, ila Msigwa alipoondoka yeye akabaki na CHADEMA.
 
Una umri gani hadi unapata ujasiri wa kuniita dogo? Usiwe mjinga wa kudhani kila aliyomo humu ni kijana mdogo tu.
Wewe ni dogo kutokana na unachoandika utakuwa umemaliza form four mwaka jana. Usibishe. Au ndo upo form four now.
 
Back
Top Bottom