Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,168
- 5,522
Kada wa chama cha mapinduzi CCM Bwana Abdallah kambaya Amesema chama hicho kinajenga hoja kwa misingi ya Sera Katika kuwahudumia wananchi wake
Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wananchi wa kijiji cha mtumbikile kata ya kilangala huko manispaa ya Lindi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni Katika Jimbo la Mchinga.
Amesema Katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wa Rais Samia wananchi wameshuhudia Maendeleo mengi Katika Maeneo Yao kulingana na vipaumbele vyao huku akiwasihi wananchi kuendelea kuwa na Imani na chama cha mapinduzi CCM
Akizungumza kwa niaba ya mbunge wa Jimbo hilo Mama Salma Kikwete Katibu wa mbunge bwana Abdala mkokoe Amesema kwa kipindi cha miaka minne Jimbo hilo limepokea kiasi cha shilingi Bilioni 81.6 kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha mtumbikile wamemshukuru mbunge wa Jimbo hilo Mama Salma kikwete pamoja na Serikali kwa kuwapelekea miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya maji, Zahanati, shule na barabara.