A-level au Diploma?

Apr 6, 2015
36
15
Nina mdogo wangu kamaliza form four mwaka jana (2015) na amepata division one ya point 12 na angependa sana kuwa daktari. Sasa naombeni ushauri wenu wakuu, ipi ni njia sahihi kwake maana kuna option mbili:
1/ Aende A-level akasome PCB
Hili jambo linanitatiza sana, maana anaweza kwenda A-level na mambo yakawa sio mazuri sana (God forbid) na mwisho wa siku anaweza kuishia kupoteza miaka miwili au akajikuta anapelekwa kozi ambayo haitaki (tofauti na udaktari) chuo kikuu kutokana na performance yake.

2/ Diploma in Clinical Medicine
Nimpeleke akachukue diploma ya clinical medicine miaka mitatu maana ana qualifications zinazotakiwa (ana C ya Physics, B ya Chemistry na A ya Biology pamoja na A ya Basic Mathematics). Ambapo akimaliza ndo ajiunge na Doctor of Medicine (MD). Hii itakua imemsaidia kufuata njia yake anayoitaka bila kupoteza muda au kuhofia kufuata njia nyingine kutokana na performance ya kidato cha 6.

Msaada wenu wa mawazo na ushauri wadau tafadhali.
 
Mpeleke Advanced kwa ushauri wangu huyo dogo yuko vizuri sana tena kama uwezo upo peleka private school atabutua vizuri sna
 
Peleka Dip,,,kaka hata Mimi katika Maisha yangu sitakuja kuruhusu damu yangu yeyote kwenda A level in kupoteza muda hususani Kwa MTU smart kama Mdogo wako,,,
 
Kwa aliyesoma PCB ataelewa nachokisema,shule ni ngumu inahitaj juhudi mazingira rafiki pamoja na bahati yani necta wamekujaje na mfanyamtihan kajiandaaje unaweza kuwa deep pepa likaja kushoto kwa PCB unapotezwa mazima,kuna faida mbili kwenda Dip ya C.O
1:uhakika wa dogo kutimiza ndoto zake kwa kumvusha kihunzi cha PCB necta
2ogo akimalza atapata ajira mapema miaka 3 mbele atakuwa na kipato chake na atasoma MD bila stress
 
Kama uwezo wa shule anao peleka advance akasome ila akmaliza chuo ana uwezo wa kuchagua course aitakayo anaweza akabadli mawazo course nyngne zaid ya MD..Ila msklize yey anataka nn kwanza kam yey anatak dip,mpeleke uko maana kwa combination hizi za sayansi PCB au PCM mambo huwa tofaut na o'level ukjisahau kdogo tu ata kam o'level ulkuwa bright unaweza usiamin
 
Mkuu kwanini kwa ufaulu huo unaogopa dogo kwenda kusoma alevo??? Kwa ushauri tu dogo anauwezo..mpe moyo mjengee morali hakika hutajuta!!!

Je amepangiwa shule gani??? Kama mnauwezo mpeleke private

NB: Muulize kwanza yeye anataka nini! Akisema alevo mwache aende...usiwe na wasi wasi nae!!
 
Na kwanini ujisahau???
 
Kama wewe pcb ilikukimbiza usizani kila mtu inamshinda!! Kama anauwezo atafaulu vyema tu!! Kama hana hata akienda huko diploma watamla kichwa!
 
Peleka Dip,,,kaka hata Mimi katika Maisha yangu sitakuja kuruhusu damu yangu yeyote kwenda A level in kupoteza muda hususani Kwa MTU smart kama Mdogo wako,,,
Nimesoma alevo mpaka leo sijuti!! Kama hukua serious na masomo usiwekee vikwazo wenzako!!
 
mdogo wangu pia anataka kua daktari na nimemshauri aende Diploma na tume apply Muhimbili,Lugalo na KCMC (Ordinary Diploma of Clinical Medicine ) naona hii ni njia rahisi na ita mpa uelewa mpana wa kile anachotaka kusomea tofauti na mtu alietokea Form 6 ajui chochote kuhusu anachotaka kusomea yani ananza upya wakati wa Diploma anakua na uelewa mpana zaidi.Kwa ushauri wangu mwambie apply Diploma
 
mpeleke chuo.,huko advance asipokuwa makini,baadae huko chuo atajikuta anasoma facult tofauti na MD,
 
Rout #1 Advance PCB
Rout #2 Clinical officer
Aisee asikuambie mtu rout no 2 ni fupi na nismooth kufika destination yako.
Rout no 1 ni ndefu na inamabonde na miinuko mingi muno, usitishwe na ufaulu wa olevel biology ya advance haitabiliki. Ni nyepesi kuisoma na kuilewa lakin sio kuijibia mitihani na hakuna kitu kupya utakachokisoma ambacho hujakisoma olevel.
 
Nielewe nini wakati hamna cha kuelewa?

NB: Si kila mtu JF ni mtoto mwenzako jitahidi kuwa na hekima.
Hebu angalia wengi wanasuggest nn kati ya dip na advance level,,,next time sihitaji malumbano ya kijinga,,,
 
mi nashauri apite diploma. nimesoma PCB na kuna mtu alikuwa na 12 ila six alichemka ila hii siyo sababu ya msingi sana.
 
Nishawah soma PCB! Naitambua! Naielewa! Dogo Kama Hana Mapenz Na Mishe Za Ajabu Na Anajiamin Mpeleke!! Mi nilisoma nikapata 0! Nikarud 2 steps below! Nikasoma Diploma Ya Co Hatmae Degree Ya Clinical Officer And Surgery Pale Kenyata University!! Now napishan kweny korido na watu wa MD salary Different 300k! Sijutii Kufel Kwangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…