4R = 4 x Reverse

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
14,360
53,812
1R =Reverse katika usalama wa wananchi
TLS wametoa taarifa ya waliotekwa, zaidi ya asilimia 90 ya walioripotiwa kutekwa katika ripoti hiyo, wametekwa toka mwaka 2021 kipindi cha utawala wa awamu ya 5(b) ya Samia, hii inaonyesha hali mbaya ya usalama wa wananchi, na hii ni reverse mbaya zaidi maana usalama wa wananchi ni priority

2R = Reverse kwenye ustawi wa maisha ya wananchi
Hali ya maisha ya wananchi inazidi kuwa mbaya. Kipato cha mwananchi kinazidi kupungua, ubora wa elimu unashuka, kipato cha mwananchi kinazidi kupungua. Huku matumizi ya serikali yakizidi kuongezeka.

3R= Reverse katika utawala bora unaofuata sheria
Katika kipindi cha miaka michache ya utawala wa awamu ya 5(b) angalau kuna progress kidogo ilianza kuonekana lakini sasa hali hiyo imechange sasa hivi
tunaona polisi bila aibu wanapiga viongozi wakubwa wa vyama vya upinzani, hii ni aibu isiyo na mfano. Polisi inayojielewa itavamiaje ktk ofisi za chama kutwaa funguo kibabe kisha kesho yake kuvunja ofisi hiyo?. Hii ni ajabu sana

4R= Reverse katika kulinda rasilimali za nchi
Leo tunaingia mikataba mibovu zaidi, sheria ya kulinda rasilimali haiheshimiwi, tunaingia mikataba mibovu kama ya misitu, bandari na radilimali nyingine. Hii kitu ni hatari mno

Kwa kweli hizi 4R zimegeuka Reverse x4 , haziwasilishi progress zaidi ya kupiga hatua kurudi nyuma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…