Kuelekea michezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya kombe la Afrika (AFL) kesho kati ya Simba SC dhidi ya wenyeji Al Ahly, katika dimba la Cairo imebainika kuwa sheria ya goli la ugenini sio ishu tena.
Wawili hao walipelekeana moto kwa sare ya 2-2 katika dimba la Benjamin Mkapa huku wengi wakidhani Al Ahly wangefaidika na magoli mawili ya ugenini lakini sasa pambano hilo litaanza upya katika dimba la Cairo.
Taarifa ya CAF baada mechi hiyo iliyoshuhudia Simba SC ikitoka nyuma na kuongoza kwa dakika tatu kufuatia magoli ya Kibu Dennis aliyefuta bao na Reda Slim na Sadio Kanoute aliyeipatia Simba SC bao la uongozi kabla ya Mahmoud Kahraba kuisawazishia Al Ahly dakika tatu baadae, faida ya goli la ugenini halihesabiki tena kwenye AFL.
Sehemu ya taarifa ya CAF ilisema; “Kwa kuwa mabao ya ugenini hayahesabiki mara mbili tena, sare hiyo inaning'inia vyema kwenye mzani kuelekea mechi ya marudiano nchini Misri wiki ijayo.”
Je, mnyama atatoboa kwenda Nusu fainali?