Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
Aboubakar Ally alienda kamati ya malalamiko ya TCRA kulalamikia suala la kupokea sms kutoka Umojabet bila ridhaa yake. Suala hilo alilalamika Voda lakini hawakuchukua hatua.
Walipofika kamati ya malalamiko Vodacom walikubali kuwa mteja wao alikuwa anapokea sms hizo lakini wao hawahusiki na utumaji wa sms hizo.
Hata hivyo walikiri kuwa Umojabet ni mteja wa bulk sms lakini hawawauzii wateja hao wa bulk sms namba za kuwatumia watu matangazo.
Hata hivyo walishindwa kusema kwa nini walishindwa kuchukua hatua ya haraka ya kuzuia sms hizo mara baada ya mteja kulalama.
Kwasababu ya usumbufu, Vodacom waliamriwa wamlipe Aboubakar Ally Tsh 1,500,000 kwa usumbufu pia wamtumia ujumbe wa kumuomba radhi.