14 wafariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bango kuanguka India

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,286
50,360
Takriban watu 14 wameaga dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bango kubwa kuanguka wakati wa dhoruba ya ghafla katika mji wa Mumbai nchini India.

Bango hilo, lenye ukubwa wa mita 70 kwa 50 kwa mujibu wa polisi, lilianguka kwenye nyumba na kituo cha petroli jijini siku ya Jumatatu.

Huduma za dharura zinasema watu wachache bado wamenaswa chini yake na shughuli ya uokoaji inaendelea.

Serikali ya jimbo la Maharashtra, ambako Mumbai iko, imeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu tukio hilo.

Picha kwenye chaneli za habari za nchini zinaonyesha bango kubwa likiyumba kwenye upepo kabla ya kuacha njia na kuanguka kwenye majengo karibu na barabara yenye shughuli nyingi katika kitongoji cha mashariki cha jiji cha Ghatkopar. Magari kadhaa yalipondwa katika ajali hiyo.

Katika picha kutoka eneo la tukio, timu za dharura zinaweza kuonekana zikiondoa mabaki. Kanda za video zinaonyesha wafanyakazi wa uokoaji wakimtoa mwathiriwa kutoka chini ya ubao ulioanguka na kutumia zana za nguvu kukata chuma.

"Tumeokoa karibu watu 80 salama," afisa mmoja aliambia shirika la habari la ANI. "Kuna gari moja jekundu ambalo limeharibika vibaya, tunashuku kuna baadhi ya watu wamekwama ndani.

7c2556e1-b11f-4928-9dbb-ac52645d37c5.jpg
 
View attachment 2990014
Bongo mpaka lizike watu kama 100 hivi halafu tutume salamu za rambirambi na kupotezea na mechi ya Yanga Vs Simba.
 
Kuna Nchi yenye Muungano wa kihuni imemuweka rais wao Kila mkoa,wilaya kata hadi vijinini huko na kuwa kama uchafu.wanasubiri maafa kama haya.
 
Kwa watu wenye akili, hiyo ajali itatumika kama somo la standards za uwekaji mabango na wapi yawekwe na kutungiwa kabisa Sheria ambayo mtu akiivunja anachezea fine kali, na miezi kadhaa jela.

Sasa nitashangaa sana kama hili tukio halitawapa somo hawa ng'ombe na kuchukua hatua za haraka sana kuyafuatilia mabango mengine yaliyowekwa kihasara hasara.
 
Takriban watu 14 wameaga dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bango kubwa kuanguka wakati wa dhoruba ya ghafla katika mji wa Mumbai nchini India.

Bango hilo, lenye ukubwa wa mita 70 kwa 50 kwa mujibu wa polisi, lilianguka kwenye nyumba na kituo cha petroli jijini siku ya Jumatatu.

Huduma za dharura zinasema watu wachache bado wamenaswa chini yake na shughuli ya uokoaji inaendelea.

Serikali ya jimbo la Maharashtra, ambako Mumbai iko, imeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu tukio hilo.

Picha kwenye chaneli za habari za nchini zinaonyesha bango kubwa likiyumba kwenye upepo kabla ya kuacha njia na kuanguka kwenye majengo karibu na barabara yenye shughuli nyingi katika kitongoji cha mashariki cha jiji cha Ghatkopar. Magari kadhaa yalipondwa katika ajali hiyo.

Katika picha kutoka eneo la tukio, timu za dharura zinaweza kuonekana zikiondoa mabaki. Kanda za video zinaonyesha wafanyakazi wa uokoaji wakimtoa mwathiriwa kutoka chini ya ubao ulioanguka na kutumia zana za nguvu kukata chuma.

"Tumeokoa karibu watu 80 salama," afisa mmoja aliambia shirika la habari la ANI. "Kuna gari moja jekundu ambalo limeharibika vibaya, tunashuku kuna baadhi ya watu wamekwama ndani.

View attachment 2990014
Hawa si ndio watetezi wa magaidi wa kizayuni! Balaa hilo
 
Back
Top Bottom