Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema limesikitishwa na taarifa za wakimbizi wanaokimbia mapigano Kaskazini mwa Msumbiji kulazimishwa kurudi nchini kwao baada ya kuvuka mpaka kuingia Tanzania.
UNHCR imesema imepokea shuhuda za maelfu ya wakimbizi waliorudishwa...