Ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa nyenzo muhimu katika kujifunza maarifa fulani ni lugha, lugha ndiyo hutumika kuhifadhi maarifa mbalimbali lakini pia ndiyo njia ya mawasiliano. Kila taifa lina lugha zake maaulumu za kufundishia kutokana na sababu mbalimbali walizojiwekea wao kama nchi...