Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Akhaaa! Hata kama Mahakama haitendi haki, hakuna anayeruhusiwa kutoa hukumu kati ya pande mbili zinazozozana au kogombania haki flani, ni Mahakama pekee. Tunapaswa kurekebisha mfumo wetu wa haki kama tunaona hautendi haki na sio waziri kuingilia. Ndio maana CCM wanaingilia uchaguzi na kuamua nani ashinde na kwa kura ngapi na nyie watanzania mnaona poa tu. Watanzania wengi ni watu wasio na akili nzuri na wanyonge sana.
Basi kama unaona waziri kavunja katiba,nenda Mahakamani kamshitaki,.alafu Mahakama ndiyo itasema kama kweli waziri ana.makosa,na siyo wwe.kutuaminisha utakavyo wwe!!
 
Hata huyo aliyedhulumiwa na Mmasi alishinda kesi Mahakamani, sema Mmasi akawa mbishi tu kutii Hukumu ya Mahakama Kuu!!
Hukumu ya mahakama inafanyiwa kazi na mahakama yenyewe, huo ni muhimili unajitegemea, hauhitaji msaada wa waziri au mtendaji wa mtaa, una court brokers
 
Salaam, Shalom!

Nimefuatilia Kwa ukaribu jinsi waziri Jerry Slaa anavyofanya katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, japo Bado ni mapema sana kusema kuwa anafanya vizuri, lakini Kwa sasa itoshe kusema ana kitu kinachoonekana, na atafika mbali, tuendelee kumwombea.

Nimesikiliza Kwa Umakini jinsi alovyotatua case ya Tajiri aitwaye Mzee Mmassy aliyenunua nyumba Kwa marehemu aliyeko kaburini, yaani document zinaonyesha marehemu akiwa kaburini alisaini mauziano na kumuuzia nyumba tajiri Mmassy, na jinsi alivyotatua case Ile kwa uwazi Kwa kutumia nyaraka halali katika ofisi ya ardhi, na jinsi alivyoweza kuwarudishia nyumba watoto na mke wa marehemu nyumba Yao, kiukweli Mungu aendelee kumjalia uhai na AFYA na baraka kiongozi huyu.

Nilifanikiwa pia kufuatilia jinsi alivyosaidia kutatua mgogoro ulioletwa na Msama, Kwa kutomtendea HAKI yake mama yule aliyedai kiwanja chake, pia nimeona ufuatiliaji, uthubutu na uchapakazi wa Waziri huyu kijana Jerry Slaa.

Ni maombi yangu, akae chini na viongozi wenzie katika wizara yake na kuja na mpango MIKAKATI wa kutatua migogoro ya ardhi Nchi nzima bila kuwepo haja ya kusafiri huku na huko, uwepo mfumo mzuri na WA haraka zaidi kuwafikia wananchi na kutatua migogoro hiyo ya ardhi.

So far, KAZI imeonekana inafanyika,

Mungu Mbariki Waziri huyu Jerry Slaa,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Ameeen.

Source: Milard Ayo tv.

Karibuni🙏
Huyo muigizaji tu hana lolote. Wazir badala ya kusimamia sera anagawa hati? Asijue kwamba hati na migoro ya ardhi ni matokeo ya sera mbovu
Atuambie tangu ile clinic ya maigizo kafanya tena wapi na amebakisha wapi na wapi ili amalize kugaawa kote Tanzaniq?
Asitufanye wajinga bhana
 
Hukumu ya mahakama inafanyiwa kazi na mahakama yenyewe, huo ni muhimili unajitegemea, hauhitaji msaada wa waziri au mtendaji wa mtaa, una court brokers
Sasa kama hati miliki ya ardhi umepewa na Commissioner wa Aridhi ,sasa Commissioner anashindwaje pia kukukabidhi eneo lako,maana yeye ndiyo analijua vizuri sana kuliko hiyo Mahakama unayosema!! Nenda kasome mamlaka ya Commissioner wa Aridhi, na utaelewa majukumu yake kisheria!!
 
Sasa kama hati miliki ya ardhi umepewa na Commissioner wa Aridhi ,sasa Commissioner anashindwaje pia kukukabidhi eneo lako,maana yeye ndiyo analijua vizuri sana kuliko hiyo Mahakama unayosema!! Nenda kasome mamlaka ya Commissioner wa Aridhi, na utaelewa majukumu yake kisheria!!
Nilichogundua ninabishana na mtu wa shule za kata
 
Erythrocyte anahoji,

Lini utatatua mgogoro wa CCM kupora na kujimilikisha Mali za umma kama viwanja vya mpira kama CCM kirumba nk nk?
 
Waziri Slaa, kama umeanza kuwagusa pia wa ndani ya chama chako,

Hapo Kweli utauona mzizi wa fitna,

Utajua kiini Cha matatizo ya ardhi Nchi hii.

Cc: Erythrocyte
 
Back
Top Bottom