Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,966
- 46,736
Hali ya maisha nchini imezidi kuwa ngumu zaidi, hali ni ngumu zaidi kwa familia zenye watu wengi ambao ni tegemezi kwa angalau wanafamilia wachache wenye kipato ambacho nacho ni kidogo. Matokeo yake watu wengi wamekuwa wakiishi maisha ya mkononi kwa mdomoni tu "hand to mouth" kwa sasa jambo ambalo ni hatari sana.
Mwaka 1980 China baada ya kuona idadi ya watu wake inaongezeka kwa kasi huku kiwango cha umaskini bado kikiwa juu na ikiwa na malengo makubwa ya maendeleo ilianzisha sera ya mtoto mmoja kwa familia moja. Sera hiyo ililegezwa mwaka 2015 ambapo familia ziliruhusiwa kuwa na watoto hadi wawili.
Kwa sasa wastani wa mwanamke kuzaa watoto Tanzania ni watoto 5! Hiki ni kiwango mara mbili zaidi ya wastani wa kidunia. Hiki ni kiwango kikubwa sana kulinganisha na hali ya uchumi ya raia wengi. Hali hii inachangia kuzoretesha kasi ya maendeleo, kuongeza ugumu wa maisha na umaskini kwa kiasi kikubwa.
Ni wakati wa sasa serikali ya Tanzania kulipa umuhimu jambo hili na kuja na sera mahususi ya kuhamasisha wananchi kutozaa watoto zaidi ya wawili. Watoto wawili iwe ni ukomo hadi hali ya uchumi itakopukwa nzuri.

Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana. Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yaani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi. Hizi shule unakuta...
www.jamiiforums.com
Kusafiri na watoto wadogo 1-8 ni kero
Hii wiki nzima nimekua kwenye safari ya mikoa ya Kaskazini, Nyanda za juu kusini mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa, kwa kutumia (public transport) mabasi ya mikoani niliona kero kubwa ya baadhi ya wasafiri kusafiri na watoto wadogo na hawako tayari kuwalipia seat. Hii niligundua ni kero kwa mzazi...
www.jamiiforums.com